Pages

Friday, August 3, 2012

Mama salma kikwete tukumbuke wenzio

Kwako Mama Kikwete, Saalam,
Pole kwa majukumu mengi uliyonayo mimi binafsi nakutakia mfungo mwema wa Ramadhan na nina imani mwezi huu utakua na manufaa mengi kwako na kwetu kwa ujumla MAANA UTATUOMBEA WALIMU WENZIO.

Pamoja na salamu hizi napenda nieleze wazi kuwa mzee alipata kura nyingi zetu walimu kutokana na wewe, ndo maana tulidiriki kumwita shemeji yetu, tuliamini urais kuwa kwake utakua kwako pia na hatimae kwetu walimu wenzio. Tulijua tuna mtu wa kutusemea sasa ambae ni wewe, Tulijua unayajua vema maisha ya walimu wenzio na kwamba utapata muda wa kumshauri baba kuhusu kundi hili ambalo wewe ulikua mdau kwa muda mrefu.

Mzee wakati wa kampeni mwaka 2005 nakumbuka alikua Mwanza alisema serikali yake itamaliza matatizo ya walimu nao
wabaki na kazi ya kusomesha watoto tu. lilikua jambo lililoibua hisia za walimu wengi, na kwakweli tulikua tayari kufa na shemeji yetu. alishinda vema naamini walimu wengi walitoa uungaji mkono nikiwemo na mimi. Dada/mama taaluma hii bado ina hali mbaya maisha yetu yamejaa mashaka, tumeshindwa kupata milo mitatu kwa siku, tumeshindwa sasa kulipa ada za watoto wetu mashuleni, tumekopa kila pahala penye kukopesha ili tuweze kupata ada za wanetu ambao wanaunyafuzi kutokana na milo duni tunayoawalisha kutokana na uwezo wetu mdogo. Wapo wenzetu wanapata mshahara sh 0/= kutokana na mazingira kama hayo niliyoeleza hapo juu!

Tumejaribu kuyaeleza haya kwa muda mrefu bado hatujapata faraja wala nafuu, chama chetu cha walimu kikajaribu kuhangaiika kuona kama tunawez kufikiriwa, na hatimae tupate aheri. wameenda mahakamani hapakutokea mabadiliko, ikabidi watangaze mgomo ambao kwakweli tulitamani mzee na wewe msikie walimu wanamateso gani huku kwenye profession yako bado nako tumechinjiwa baharini
1/8/2012 mzee akatoa hotuba nzuri sana ingawa ndani yake tuliona hukumu itakauaje siku ya leo tarehe 2/8/2012, mama wakati tukisubiri hukumu wengi walitubeza kuwa hukumu tayari imetolewa na mzee na mahakama itatimiza unabii tu! Nikweli imekua hivyo.

Mama/dada unaweza ukaona tunavyohangaika ili kupata nafuu ya maisha katika nchi hii ambayo inaongozwa na mtu aliyeoa dada yetu itakuaje akija mtu ambae hana kabisa uhusiano nasi? Natamani sana mwanangu au ndugu yangu asijiingize kwenye taaluma hii maana haithaminiwi tena na wala haionekani kama ina umhimu wowote.

Mama kwani wakati mnapoongea na mzee kwa masuala ya kifamilia au ya kitaifa huwezi kumshauri walau awe na huruma kwa kaka na dada zako sisi? Naamini ukijipa assignment ya kufanya hivyo kila jioni utatuokoa na kwakweli hata baada ya 2015 tutakukumbuka kwa kutupigania.

Mwisho dada utakapokua kuwa ukila na kunywa hapo magogoni, ukumbuke wenzio huku hata kuamkia mhogo au kiazi haiwezekani tena maana hata mvua hazinyeshi vizuri hata mavuno hatupati kwenye vishamba vidogo tunavyomudu kukodi vijijini,
Utakapo kuwa ukilala na kusinzia ukumbuke wenzio tunafukuzwa na wenye nyumba kwa kukuchelewa kulipa pango la nyumba za udongo tulizopanga kutokana na kutokuwepo kwa nyumba mashuleni. Aidha utakapo kuwa ukisafiri kwenye ile ndege ndani au nje ya nchi, tukumbuke wenzio hata matairi ya baiskeli zetu yameisha tunasubiri mshahara walau tununue mengine ili tujiepushe na pancha za mara kwa mara.

ujapoita watoto yatima na wanawake kuwafuturisha jioni hapo pembeni ya bahari tukumbuke wenzio hatuna hata uwezo wa kutoa mchango wa rambirambi mtaani ila tunakopa kila misiba inapotokea tukisubiri mwisho wa mwezi.

Mama/dada najua unafahamu kuwa kile ambacho kingetupa kipato kidogo ni kuuza ubuyu na barafu lakini tumezuwiwa na walimu wa kuu. Tumetii yote hayo tumejaribu tuiition bado madiwani na wazazi wametushtaki. Tumeshindwa kote sasa TUNAKUANGALIA WEWE TU. Tafadhali fanya haraka kumshauri mzee vinginevyo utatukuta tumekufa kwa njaa, shinikizo la damu au utapiamlo. Utakuta ndugu zako huku hatuna tumaini hata stori hatutakupa juu ya maisha ualimu uliyoyaacha kwa miaka 10.
Nakutakia maisha mema na utetezi mwema wa walimu wenzako.

Mwalimu Mpole

Popular Posts