Mshiriki  wa Shindano la Epiq Bongo Star Search Digna Mbetela kutoka Dodoma akiwa  mbele ya majaji wa shindano hilo (hawapo pichani) walipokuwa wakifanya  mchujo mkoani Tanga katika Ukumbu wa Club La Casa Chika Julai 28,2012 na  mwana dada huyo kujitosa tena kujaribu bahati yake ya kwenda jijini Dar  es Salaam.
 Mwamko  wa washiriki katika shindano la Zantel Epiq Bong Star Search umekuwa  kama ulivyotegemewa ambapo zaidi ya washiriki 300 walikuwa wameisha  jisajiri kwanza kwa ajiri ya kufanya usaili siku ya leo.
Washiriki  wengi walioshindwa kupata nafasi katika mikoa usaili  uliopitiawamejitokeza katika mkoa wa Tanga kitu ambacho kimeongeza  ushindani kwawashiriki kutokea eneo hili la Tanga.
 Washiriki  wa EBSS wakiwa nje ya ukumbi wa Club la Casa Chika jijini Tanga tayari  kwa kufanya usaili na kupatiwa namba zao kusubiri kuingia kwa majaji.
 Mshewa  Mussa akiwakilisha tena baada ya kete yake ya awali mkoani Arusha  kugonga mwamba na kuamua kutia maguu jijini Tanga kujaribu bahati yake.
 Washiriki wa EBSS wakiwa nje ya ukumbi wa Club la Casa Chika jijini Tanga kusubiri kuingia kwa majaji.
 Faisal Jafari wa kutoka Tanga nae akisubiri kurusha kete yake kwa majaji.
Mshiriki Hidaya Hanein akiwa katika foleni ya kuingia kwa majaji