Pages

Sunday, July 29, 2012

Rais Jakaya Kikwete Afungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika Katika Kuondoa Umaskini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam jana July 28, 2012. Wa tatu toka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mhe Steven Wassira, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone Mhe Momodu Kargbo, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Mipango Dkt Philip Mpango na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo rasmi na Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam jana July 28, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian(kuhsoto) na Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing. baada ya akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Jana July 28, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipicha picha na ujumbe toka china unaohudhruia Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Jana July 28, 2012.Picha na IKULU

Popular Posts