
   Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa wilaya ya  Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo  mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11     itafunguliwa na kuwekewa mawe  ya msingi.
 
 Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salam  Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa  wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es  Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili  jijini  Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba. 
   Wakimbiza  Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest  Mwanossa (wa kwanza mbele)  wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali  ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam. 
 
  Vijana wa halaiki kutoka wilaya ya Temeke wakiimba wimbo maalum wa Mwenge wakati wa mapokezi leo jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya wafanyakazi  na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuupokea Mwenge wa  Uhuru katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO