Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB"   wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa   ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo   mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika   hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria   unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya   nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni   ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni  wadhamini  wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie)  linalozinduliwa  leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha  na Othman  Michuzi 
    Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama   aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo   Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa   Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake   cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za   Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya   Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi 
   Msanii wa Bongo Movie,Mayassa Mrisho akikabidhi Chandarua kwa Mama   aliejifungua watoto mapacha kwenye hospitali ya Bombo,Tanga mapema leo   asubuhi.Picha na Othman Michuzi.