Pages

Tuesday, June 26, 2012

Waziri wa Mambo ya ndani na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe Alipotinga Clouds FM

Pichani wa pili kutoka shoto ni Waziri wa Mambo ya ndani na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe akiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha Power breakfast,kinachorushwa na redio ya Clouds FM,Mikocheni jijini Dar,kulia ni Paul James,Barbla Hassan pamoja na Gerald Hando.
Waziri wa Mambo ya ndani na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe akifafanua jambo mapema leo asubuh kwenye kipindi cha Power breakfast kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo na suala la usalama wa Taifa letu,ikilinganishwa na mambo yanayotokea nchini Kenya na kwingineko hivi karibuni,Kulia kwake ni mtangazaji Gerald Hando akimsikiliza Mh Membe.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akisalimiana na Mh Membe mara baada ya kumaliza mahojiano yake na redio Clouds FM,kulia ni Simon Malenga ambaye ni muaandaaji wa vipindi mbalimbali wa Clouds FM.
Baadhi ya uongozi wa Clouds Media Group,ukiongozwa na Ruge Mutahaba ukiagana na Waziri Membe mara baada ya kumaliza mahojiano yake na redio Clouds FM,Mikocheni jijini Dar.

Popular Posts