*Mkutano wavurugika.
*Waunda kamati ya kusimia kijiji hicho.
*Diwani afunga mkutano.
 *******
Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe.
Wananchi  wa Kijiji cha Isyonje,Kata ya Isongole,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya  wamemvua uongozi,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Venance Daima na  halmashauri ya kijiji kizima kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali na  kutosimamia ipasanyo rasilimali za kijiji ikiwemo mianzi ya asili na  mashamba ya kijiji.
Tuhuma  hizo zimetolewa katika mkutano maalumu wa kijiji hicho uliofanyika Juni  28 mwaka huu mbele ya Diwani wa kata hiyo mheshimiwa Laurence Nyasa  Mfwango,ambapo baada ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa  na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Ambokile Kinjisi na kubaini  kuwa jumla ya shilingi 1,118,000 kufunjwa na mhasibu wa kijiji Bwana  Michael Mbilinyi.
Aidha  mhasibu huyo alipotakiwa kuonyeshwa pesa hizo zilipo alishindwa hali  iliyompelekea kukiri kosa hilo na kuahidi kuzilipa Juni 29 mwaka huu  baada ya kujiwekea dhamana ya shamba la miti.
Hata  hivyo wananchi hao waliutupia lawama uongozi wa kijiji kwa kutosimamia  mali ikiwa ni pamoja na uuzaji holela wa mianzi na ukodishwaji wa  mashamba bila ridhaa ya wananchio na kutoitisha mikutano ya hadhara  ikiwa ni kinyume na kanuni za Serikali ya kijiji.
Katika  hali isiyokuwa ya kawaida baada ya tuhuma hizo wananchi walimtaka  mwenyekiti huyo na halmashauri yake kujiuzuru,ambapo walikubaliana na  kijiji hicho kusimamiwa na kamati ya mpito,chini ya Afisa mtendaji wa  kijiji Bwana Kinjisi.
Kutokana  na wananchi kuchoshwa na uongozi  huo baadhi yao waliondoka mkutanoni  kwa hasira  na viongozi wa kijiji kuacha viti vyao na kumuacha  Diwani,ambaye alilazimika kufunga mkutano.baada ya mwenyekiti  aliyeufungua mkutano huo na wananchi wakaridhia Kamati ya watu 10  kusimamia shughuli za kimaendeleo hadi uongozi mwingine utakapochaguliwa  kwa mujibu wa kanuni za kijiji.