Pages

Sunday, June 24, 2012

Zambia waishukuru PrecisionAir kuanza Safari za Dar es Salaam / Lusaka

Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi wa safari za Shirika hilo la ndege jana kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka Zambia kupitia Lubumbash.Hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo akizungumza kaatika hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Mgeni Rasmi, Naibu Wazizi wa Usafirishaji, Kazi, Usambazaji na mawasiliano wa Zambia, Samuel Mukupa akizungumza jana katika tafrija maalum ya uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Precision Air kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka kupitia Lubumbashi. Mukupa alisema mbali ya kuzidisha mahusionao baina ya Tanzania na Zambia lakini pia itawasaidia sana wafanya biashara wa Zambia katika safari zao za kibiashara Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' Honor Janza nae alikuwepo.
Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu akiwa na Meneja Maweasiliano wa Kampuni hiyo Anneth Nkini wakati wa tafrija hiyo.
Viongozi wakishangilia jambo.
Wageni mbalimbali wakiwepo na wafanyakazi wa Precision Air wakifuatilia matukio.




Wageni mbalimbali wakifuatilia tafrija


Mkurugenzi wa Masoko, Patriki Ndekana , (kushoto), Meneja Mauzo, Tuntufye Mwambusi, Hilda Lema, Mariam Ismail na Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu wakipamba moto katika EDUDHA.


CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wake kucheza EDUDH.Picha Zote Zimeletwa na Mdau Mroki Mroki

Popular Posts