Pages

Tuesday, June 26, 2012

Nape Nnauye Ahutubia Wanachama wa CCM,Tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU)Mkoani Mbeya

Nape baada ya kuwasili mjini Mbeya kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wanachama wa CCM, tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya, katika mahafali ya kuwaaga,jana Juni 25, 2012, katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya.
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema akimkaribisha nape kuzungumza kwenye mahafali hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM Chuo Kikuu cha TEKU Boniface Paulo.
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimpa kadi ya CCM Aranora Msigwa wa mwaka wa tatu, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) alipopokea wanachama wapya wa CCM, wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la Chuo hicho mjini Mbeya,Jana June 25. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa wa CCM Mbeya, Maganga Sengerema.
Wana_CCM tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) Mbeya wakimpa zawadi ya picha yake, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye wakati wa mahafali ya wana-CCM tawi la chuo hicho.
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akishiriki kucheza muziki wa mtindo wa 'Kwaito' wakati wa sherehe za mahafali ya wana-CCM tawi ala Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) katika hoteli ya Paradise mjini Mbeya jana June 25.
Wana-CCM tawi la TEKU wakifurahi wakati wa kwenye mahafali yao yaliyofanyika uykumbi wa hoteli ya Paradise mjini Mbeya.

Popular Posts