.jpg)
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa  Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini,  Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar.  Wanafunzi hao  wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu  cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa  wameongozana na  Watendaji Wakuu wa  Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete  Ikulu  jijini Dar es salaam leo  Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa  ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na  ubalozi wa Tanzania Marekani
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu  wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini  Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya  kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na  ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama  hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema  amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama  za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio  ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu   ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.Picha na IKULU