Pages

Monday, June 25, 2012

Tawi la Chadema Washington DC limepokea Mwanachama Mpya Ambae Pia Amezawadia Tawi Hilo Zawadi ya Gari

Hussein Kauzel Msabaha akiwa na kadi ya Chadema
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi kulia.
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakimkabidhi rasmi Hussein Kauzel Msabaha kadi ya uwanachama.
Uwongozi wa Tawi la Chama Washington DC ukimkabidhi Hussein Kauzel Msabaha daftari la Sera ya Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Daftari la Sera ya Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Wanachama wa tawi la chadema Washington DC wakipata picha ya pamoja
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi, wapili kulia, akiwa na katibu Libe Mwang'ombe, kushoto, pamoja na katibu mwenezi Kosmas Wambura, wa kwanza kulia, wakiwa katika kukamilisha mpango mzima wa kumkabidhi rasmi kadi ya uwanachama ndugu Hussein Kauzel Msabaha wa kwanza kushoto, ambae amejitambulisha rasmi kuwa mwanachama wa Chadema.
Hussein Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi akionyesha funguo za gari ya aina ya Chevy Suburban walilokabidhiwa na Hussein Kauzel Msabaha
Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata picha ya mamoja baada ya kuzawadi ya gari aina ya Chevy Suburban kutoka kwa Hussein Kauzel Msabaha, baada ya kupokea rasmi kadi ya uwanachama wa Chadem jijini Washington DC
Gari ya aina ya Chevy Suburban walilozawadiwa Chadema na Hussein Kauzel Msabaha
--
Siku ya Jumamosi Juni 23, 2012, Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC lapokea zawadi ya gari aina ya Chevy Suburban kutoka kwa Hussein Kauzel Msabaha, baada ya kukabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama mpya wa chama hicho jijini Washington DC

kiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi Majimbo mengine ya Marekani.

Naye mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu kwenye kukijenga Chama.Picha na Habari na Mdau SwahiliVilla

Popular Posts