
Huyu   ndie Naomi  James  ambaye  ametawazwa  usiku  huu kuwa  Miss Redd's  mkoa  wa  Iringa na  kuzawadiwa  kitita cha  shilingi 500,000

Mshindi   wa taji la  Miss REdd's 2012 mkoa  wa  Iringa  Naomi James kati kati  akiwa na  mshindi  wa pili  Sarah  Utiku na  Catherine Mfupi  ambaye  ni  mshindi  wa tatu  mara baada ya  kutangazwa usiku  huu ndani ya ukumbi   wa Highlands mjini Iringa

Msaidizi   wa  chifu  jaji msomi Saimon  Belenge akiokoa  jahazi lisizame baada  ya wadau  wapenzi na mashabiki wa onyesho hilo kuanza  kumzomea  chifu  jaji  Bw Tasha  Jimi ambaye ni mratibu  wa Miss Redd's  mikoa ya kusini   baada ya  kuchemka kutaja namba ya mshindi  wa pili katika onyesho   hilo

Hawa   ndio  waliopenya nafasi ya tano bora kati ya  washiriki  12   waliopanda jukwani  wa kwanza  kushoto ni Amisa Zuber,  SArah Utiku,  Naomi  James ,Winfreda Felix na  Catherine Mfupi

Wadau  wa  urembo  leo  wakiwa  wamevalia  nguo  za heshima  kiasi

Warembo  wakiwa katika picha ya pamoja na washindi  na washiriki wa onyesho hilo

Mgeni  rasimi Naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gervas  Ndaki ( wa pili   kushoto) akiwa na  afisa michezo na utamaduni Manispaa ya  Iringa  Bw.Kadinde na mratibu  wa onyesho hilo Bw Dosi

Hawa ndio majaji  wa  onyesho  hilo katikati ni Tasha  Jimbo aliyetaka  kuvuruga  onyesho  dakika za mwisho

Msomi  Saimon  Belege (kulia) akicheka  baada ya  chifu jaji  kushoto  TashaJimy kuvuruga kazi  yao


Madau   Saimon  Belege  akiwa na mshindi  wa taji la Miss  Iringa mwaka  jana  na  mshindi  wa  leo katika  shindano ya  Redd's Miss Iringa Naomi James


Huyu   ndiye  Tasha  Jimy aliyezomewa kwa  kushindwa  kujua  tofauti kati ya  namba  4 na mbili hivyo  kujikuta  akizomewa  ukumbini.