Kituo  cha Redio cha Safina cha jijini Arusha leo kimeandaa kusanyiko kubwa la  neon la Mungu ambalo limelenga kuomboleza Taifa la Tanzania na  kuongozwa na kichwa kisemacho  TOBA YA TAIFA “Tubuni Dhambi zenu zifutwe” Maneno kutoka Matendo 3:19.
Kivutio  kikubwa katika mkutano huu ni pale wananchi waliokuwa wakifika hapo  wakiwa wamevaa magunia na viroba nah ii ni kutokana hasa na neon lenyewe  lilivyokuwa likiwataka kufanya hivyo. Ambalo ni “Kwa sababu hiyo  jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana  hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha”.
Mtumishi  wa Mungu, Jovin Abel Msuya kutoka Safina Radio, akitoa neon la Mungu  kwa wakazi wa Arusha na Vitongoji vyake waliofurika katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid mjini hapa leo kuomboleza juu ya taifa la Tanzania.
Umati wa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake wakiwa uwanjani hapo wakipokea neno la Mungu.
 Bibi huyu nae alijitokeza uwanjani hapo na Biblia yake akifuatilia neno na kuomboleza juu ya taifa lake la Tanzania.
 Yalikuwa ni mafundisho muhimu sana na walio na madaftari walinukuu maandiko yaliyo kuwa yakitolewa kwa tafakuri zaidi.
 Watoto nao hawakuachwa nyumbani katika maombolezo haya nao walikuwepo uwanjani hapa na wazazi wao.
 Watu  wakivaa viroba tayari kwa kushiriki mkutano wa maombolezo. Kiroba  kimoja kilikuwa kinauzwa Tsh 1,000/= na vijana wengi waliviuza sana.
 Wanahabari kutoka Star TV na ITV wa mjini Arusha wakiwa uwanjani hapo kutafuta habari za hapa na pale 
 Akina  mama ndio mara nyingi hushiriki kikamilifu katika maombolezo juu ya  tukio lolote na leo akina mama walikuwa wengi sana kuliko akina baba.
wanafunzi nao walishiriki mkutano huu wa Maombolezo juu ya Taifa la Tanzania
 Mtumishi wa Mungu, Jovin Abel Msuya akiendelea kushusha maandiko juukwaani
Jua lilikuwa lina waka na wanafunzi baade walila.








 



