Pages

Monday, August 6, 2012

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania(CAG) Kufanyia uchunguzi Taasisi za Umoja wa Mataifa

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa (UN)Bw,Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi wa hesabu za UN.
Edwin Rweyumamu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) akimkaribisha CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN)Bw,Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60 kutoka ofisi ya CAG watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Popular Posts