Ndugu zanagu, huenda mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa  nyasa na  malawi! Nilishtushwa sana na hotuba ya bwana waziri. mimi  napenda utaifa wangu  na uzalendo wangu. lakini napenda sana kutetea  mambo yangu kwa kuukubali ukweli,  kujua facts zaidi, kukubali hata zile  zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga  joja.
Eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi  zaidi  na lengo langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo  si  kubwa kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia  documents zote na  muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records  Office-Uingereza, Colonial Archives  Potsdam, ujerumani, pia malawi  national archives, tanzania national archives,  libraries za UDSM na  Chancellor college malawi. naamini ubishi utaisha kwa kuwa  documents  zote zipo.
Angalizo: ziwa nyasa liligawanywa na mabeberu wa  kiingereza, kijerumani  na kireno. mkataba wa 1890 uitwao anglo-german agrrement  unasema mpaka  wa German east africa(tz bara ya leo) na nyasaland(malawi ya leo)   unapita kandokando ya ziwa nyasa kutoka mto ruvuma mpaka mto songwe! huu  ni  mkataba wenyewe, upo ktk documents nyingi sana.....!!international  law inajua  hili na international lawyers wanaelewa nini nazungumza!  Sehemu nyingine ilikuwa  ni 1891 kati ya ujerumani na ureno, mpaka  ulianzia mto ruvuma kuelekea  Portuguese east africa(msumbijin ya leo)  na pia ureno ikawekeana mpaka na  british nyasaland(malawi)...kwahiyo,  kipindi cha ujerumani, mpaaka unasomeka 'it  passes along the shore of  the lake(nyasa).....
Mabadiliko ya mipaka:  kipindi cha kikoloni, kabla ya mjerumani  kuondoka, marekebisho ya mipaka  yalifanyika kati ya mjerumani na mreno  kwa kuspgeza mpaka mbele 0.5 KM from the  original tripartite point, na  vijisiwa vya mto ruvuma vikagawanywa. mpaka leo  ipo hivyo. na eneo  lingine ni kati ya mwingereza na mreno, ambapo, kisiwa  kilichopo eneo  la malawi linamilikiwa na msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi  lililopo  msumbiji linakaliwa na malawi. mhuo ulikuwa mkataba wa marekebisho na   ipo hivyo mpaka leo. kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na  mabadiliko haya  na hivyo hatuwezi kugombana na msumbiji wala msumbiji  hawawezi kugombana na  malawi. Mpaka wetu na malawi haukurekebishwa  popote pale mpaka mjerumani  anatoka...
Marekebisho ya mipaka kipindi cha uingereza: sote tunajua  german east  africa, sisi pamoja na ruanda na urundi tuligawanywa katika sehemu   mbili, ttukiwa chini ya League of nations tukiangaliwa na uingereza.  Kunamabo  nahitaji tuweke sawa. tukaitwa mandated territory na uingereza  ni mandatory  power. turudi ktk kamusi tutofautishe a an annexed colony  and a mandate! Mpaka  ukawekwa kati ya ubelgiji na uingereza, uliitwa  the MILNER-ORTS AGREEMENT OF  1922! katika mkataba huu, mto kagera  ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi  hivyo. Hapakuwa popote pale  ambapo eneo la ziwa nyasa lilirekebishwa kwa njia ya  mkataba baina ya  nyasaland state na tanganyika state...., isipokuwa, tofauti na  mandates  zote, tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo, mpaka wa ziwa   nyasa ukapewa wanachoitwa 'wording', na hivyo, ramani ya tanganyika na  official  records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa  nyasa! na hapa ndipo  tatizo linapoanza na sisi tumechukulia hii ndo  absolute fact, hatuendi mbele  kidogo. haya yapo pale national archives  secreatarita files, ACCESSION NUMBERE  AB 8 na AB 30! nafikiri hotuba  yote ya bwana mkubwa jana imetoka ktk files hizi,  ndizo  walizopelekewa!!!
twende mbele kidogo, ni kweli, kama  mheshimiwa alivyosema jana, ramani  nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha  mpaka upo katikati ya ziwa!  je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni  tukifikishana mbali?  hapana!mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine, japo chache  muda huu  huu na official reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo   chini. lakini ni chache! kwanini hili?bado natafuta majibu, lakini kwa   harakaharaka, unaweza ukasema kuwa uingereza ilitamani tanganyika iwe  koloni  lake na si mandate! na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata  jeshi ilisema  afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na mandate!  nahitaji tuelwe maana  ya mandate.
Hii yote ilitokea baada ya Donald Cameroon, governor wa  tanganyika  kusema kuwa tanganyika is a part of the british empire and it will   remain so! hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao  hawakuwa  wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia mapaka  wananchi wapate 'akili'  ili wapewe uhuru! kwa hiyo, kimsingi, kwa maana  ya sheria ya kimataifa,  tanganyika haikuwa part ya british empire kama  yalivyo makoloni yaliyotekwa  mojakwa moja na uingereza yenyewe! hapa  pakatokea mvutano mkubwa sana katika  house of Lords na house of  commons! na hivyo basi, mtafaruku huu wa mpaka  ulianzia hapa, kwa kauli  hii na hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu  mpaka. ipo  hivi, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipka  ya  tanganyika na ule wa ziwa nyasa! mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa   makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka  kuwekana  sawa! ndipo secretary of state for colonies alibanwa na  mjadala ulikuwa wa  kisheria zaidi ukihoji status of the mandate,  british empire, n.k; na kama  waingereza wanamamlaka ya kujipangia  kuhusu koloni waliolokabidhiwa  kuliangalia(nieleweke na si kulimiliki)!  mwishowe, mtu huyu mwenye dhamana  alisema kwamba, hata yeye anashindwa  kuelewa, 'what exactly is the sovereignty  of tanganyika lying'! jamani  mnamwelewa huyu mtu? kwamaana hiyo, haelwi vizuri  mipaka yetu, ambayo  wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'wording'!! hivyo,  tatizo linaanzia  hapa na si muda mwingine wowot!!!
Kipi hakusema bwana  mkubwa jana: kuanzia 1939, mambo yalibadilika na  hawa hawa watu tunaochukua  ashahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! na  ilipoisha vita ya pili ya dunia,  jamani oneni haya, hawa waingereza  katika ramani zao, tena nyingi  mno,(kaangalieni East africana section,  university of dar es salaam, sehemu ya  thesis, kuna cabins 3 zimejaa  ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa  na pia kutotumka  sana), kuimbezinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa  tanganyika  na nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema   hili. aliishia 1939! kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote  zikionyesha  mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! kwanini hili?natafuta  majibu, lakini nkwa haraka  naweza nikaspeculate mawili. mosi, karibu na  vita vya pili vya dunia, ilisikika  tetesi kule duniani kuwa, ujerumani  inarudi na inakuja kuchukua malokoni yake.  (kasome national archives  of tanzania, secreatariat files zote zenye kichwa cha  habari, 'the  future of tanganyika in british empire'). kwa hiyo, waingereza   walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule  mpaka  wa awali wa 1890! na pia, muda huu, baada ya kwisha vita,  tanganyika ikawa chini  ya UNO ambapo ilipewa trusteeship status!maana  ya hii ni rahisi kuliko  mandate!ilimaanisha to be granted immediate  independence! maana ya neno  immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri  yangu, waingereza wlifahamu wanatimka  mapema mno kwani mkataba unasema  hivyo....nafikiri, wakarudisha ramani  zikionyesha mpaka upo  pembeni...na kitabu ch Nyasaland cha mwaka 1958,  kinaonyesha mipaka ya  nyasaland na ziwa lote likiwa kwao! tukitaka kuwashinda  wamalawi,  lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa   kiburi na zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza.............!!!!!!!!!   !!!!  kwahiyo future of tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc  kipindi hiki,  pamoja na mipaka yake pia!! tujiulize, kwa maana ya  mandate, waingereza walikuwa  na legal authority 'kurekebisha' mpaka wa  ziwa nyasa? na je makosa waliyofanya  waingereza, ndo legal backing yetu  sisi? ebu tuzame tena tutafute facts  tuwashinde hawa jamaa!
Tulishindwana na uingereza kurekebisha mipaka.  mwalimu alisubiri mpaka  malawi iwe huru!akatoa miaka mitatu tu na asingetambua  mipaka ya  kikoloni(soma hansard, 1962). walipopata uhuru, kukawa na matatizo   ambayo jana bwana mkubwa aliyaeleza. nampongeza ni dhahiri, 1964 cabinet  crisis  ya malawi na wale mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa,  banda akaona  ziwa ni infiltratio route! sera zetu za mambo ya nje  zilikuwa tofauti. tulikuwa  frontline state kwa ukombozi, wenzetu  wakasapoti makaburu na wareno na wakawa na  balozi sehemu  hizo.....wakagombana na mwalimu, military show down miaka ya  1967-8;  matusi na kejeli zikatawala kati ya mwalimu na banda, sisi na   malawi.....kipara cha banda kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini,  mwalimu  akasema mpaka a sensible leader akitokea malawi ndipo  tutajadili tena swala hili  na si na kamuzu banda! tulikuwa kimy, na  kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo,lakini  si kusema kuwa tulitatua tatizo  la mpaka!
Tulikaa kimya!mipaka  haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo  ikitokea spark ni explosion!  Tuliirithi kupitia Article III ya OAU  CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA  WENGI WAKARIDHIA TUIRITHI,  uti possidetis, ita possidetis principle (so as you  exist, so may you  exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia  principle,  border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na  kuangalia  kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza   leo!!!
Way forward! naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza! moja ni kwa   majadiliano ya kawaida yaani diplomacy kama bwanamkubwa alivosema jana.  pili ni  kupigana vita. (war is another means of diplomacy), mnataka  kuniona kichaa!huo  ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa  kwa uganda na sis. tatu ni  mahakama ya kimataifa yaani International  Court of Justice! hapa ninawasiwasi.  kama facts zenyewe ni zile za jana  tu, sijui kama tutatoka.tutulie, tuite  wataalamu wetu wajikite ndani  sana. ni kweli kama alivyosema jana bwana mkubwa  kwa kunukuu kesi  nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama  ile sisi  ndo tutashinda!!!ninashaka....tume  jipa favour ya verdict! kabla ya   kesi.sijui.ninashaka kubwa!kunakushinda, kushindwa au suluhu!ninashaka  tena na  tena!
mimi nimzalendo,nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza  kichwa,  tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa  hoja.....!!!!
Wasiwasi: inasemekana kuna mafuta ziwani!!! kwahiyo mjue  marekani na  washirika wake hawako mbali! tujue operation ya military imperialism  na  huyu mama, mpwa wa kamuzu banda, anapata wapi hiki kiburi...nyuma yake  kuna  nini na nani!!1tuangalie haya pia.
Hitimisho. tusiwe na hoja moj tu  mkononi kama ndo water-tight evidence.  tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na  hoja nzuri ni zile zinazopingana  nasi na tusizozipenda, tukizielewa na  kuzikubali ndipo tutajipanga  namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui  yetu.....MUNGU IBARIKI  TANZANIA!ZIWA  NYASA!WANYASA!WATANZANIA!
Tusing'ang'anie tu REPARIAN LAW!
Source:  wavuti - wavuti
                      -