Meya  wa Manispaa ya Ilala, Mstahiki Meya Jerry Silaa leo aliandaa futari  iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo viongozi wa dini, viongozi wa  serikali, madiwani, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida na kufanyika  katika ukumbi wa jiji wa Anatoglo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  Pichani ni Meya Slaa akigawa tende kwa watu waliofunga.  
 Mustapher  Hassanali akiongoza wafanyakazi wa 361 kuandaa zawadi kwa wageni  waalikwa. kampuni hiyo ndio iliyoratibu shughuli nzima ya kufuturisha.
 Mstahiki Meya Jerry Silaa akimkaribisha Dr. reginald Mengi katika futari hiyo.
 Dr. Reginald Mengi akisalimiana na  SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum
 Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwakaribisha wananchi waliohudhuria futari hiyo aliyo wandalia.
 Waumini wakiwa katika swala
 Wageni waalikwa wakipakua futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Ilala.
 Viongozi mbalimbali wakifuturu.
 SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, akitoa neno la shukrani kwaniaba ya waalikwa wote.
 Mstahiki Meya, Jerry Silaa akizungumza wakati wa kufuturisha.
 Duaa ilisomwa na SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, huku Mstahiki Meya Jerry Silaa akiipokea.
 Mstahiki Meya akitoa zawadi kwa wageni mbalimbali waalikwa.
Mstahiki  Meya wa Manipaa ya Ilala, Jerry Silaa (kanzu jeupe) akipiga picha ya  pamoja na vijana wa 361 waliofanikisha shughulihiyo ya kufuturisha.