Pages

Thursday, July 26, 2012

KATA YA KWADELO YAJIKITA KATIKA KILIMO KWANZA

Diwani Kata ya Kwadelo Kondoa mkoani Dodoma Alhaji Omar Kariati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya wakulima wa kata hiyo kukabidhiwa matrekta mannem kwenye Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es Salaam, leo. Julai 26, 2012.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo za trekta, mkulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani, katika hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta manne wakulima kutoka kata hiyo, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni wakulima wa kata hiyo ya Kwadelo, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (wapili kushoto) na Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.
Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omar Kariati wakati wa hafla ya wakulima wa kata hiyo kukabidhiwa matrekta mannem kwenye Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es Salaam, leo. Julai 26, 2012.
Mkulima wa Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Gaberiel Galahenga akimkabidhi barua Diwani wa Kata hiyo, Omari Kariatikwa ajili ya diwani huyo kumpelekea kama shukurani Mkuu wa JKT, kwa shirika la Suma JKT kuwawezesha wakulima wa kata hiyo kukubali kuwapa mattekta wakulima wa kata hiyo kwa nusu ya bei na kisha kumalizia pole pole. Wengine katika picha ni, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (watatu kushoto) na Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta manne, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.

Popular Posts