Pages

Saturday, July 28, 2012

MKUTANO WA WADAU NA WATENDAJI WA MASHIRIKA YA UMMA

Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa akifungua mkutano wa siku moja wa wadau na watendaji wakuu wa Mashirika ya Umma unaojadili rasimu mapendekezo ya rasimu ya sheria mpya ya msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Msajili wa Hazina Elipina Mlaki akiwasomea wajumbe baadhi ya mapendekezo yaliyomo katika rasimu ya sheria mpya ya msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa mkutano wa wadau na watendaji wakuu wa Mashirika ya Umma uliokuwa unajadili mapendekezo ya rasimu ya sheria mpya ya msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa akisalimia baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa wadau na watendaji wakuu wa Mashirika ya Umma unaojadili rasimu ya mapendekezo ya sheria mpya ya msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wadau na watendaji wakuu wa Mashirika ya Umma waliokuwanajadili rasimu ya mapendekezo ya sheria mpya ya msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam.

Picha na Tiganya Vincent, Dar es salaam.

Popular Posts