
 002: Msaidizi  wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Josephat Sura akiagana na Meneja Mahusiano  ya nje wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim wakati Meneja huyo  alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa.
 
  Mkuu wa  Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa akizungumza na Meneja Mahusiano ya Nje  wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim alipomtembelea ofisini kwake kwa  lengo la kusalimiana na kumpatia taarifa rasmi  za hafla ya kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 inayoandaliwa na Vodacom Foundation jijini humo.
 
  Meneja  Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim akizungumza moja  kwa moja na wakazi wa Mji wa Tanga na mikoa ya jirani kupitia kituo cha  Radio Mwambao FM kuhusu futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa  watoto yatima zaidi ya 500 wa jijini Tanga leo Jumatano Julai 25, 2012.
 
 Meneja  Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu akifafanua jambo  kwa Meneja wa Radio Mwambao FM ya Jijini Tanga Bw. Hashim Gulamwa  (Katikati) na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule  wakati maofisa wa Vodacom walipotembelea kituo hicho leo Jumatano Julai  25, 2012 na kuzungumzia program ya Vodacom Foundation ya Ramadhan Care  & Share 2012 inayolenga kufuturisha watoto yatima sehemu mbalimbali  nchini wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  -- 
  Kampuni  ya Vodacom Tanzania leo inafuturisha zaidi ya watoto mia tano kutoka  madrasa za mjini na nje ya mji wa Tanga katika viwanja vya Ma-awal  Islamic ikiwa ni uzinduzi rasmi wa utaratibu wake wa kila wakati wa  mwezi mtukufu wa Ramadhan wa kujali na kuonesha upendo kwa watoto yatima  na makundi yasiyojiweza kwenye jamii – Ramadhan Care & Share
  Futari  hiyo inayoandaliwa na Vodacom kupitia kitengo chake cha misaada kwa  jamii – Vodacom Foundation itahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa  dini ya kiislamu na viongozi wa serikali mkoa wa Tanga
  Mapema  jana Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Gallawa alitoa baraka zake  kwenye futari hiyo alipotembelewa ofisini kwake na Meneja Mahusiano ya  Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim na Meneja Mahusiano kwa Umma Bw. Matina  Nkurlu kwa lengo la kusalimiana.
  “Utaratibu  wa kuwakumbuka yatima ni utaratibu mzuri nawapongeza Vodacom kwa upendo  wenu nasikitika sana kwamba sitokuwepo kama nilivyowaeleza wakati  mliponitumia ujumbe wa mualiko kwamba nitakuwa safarini Wilayani Handeni  kikazi, ila nawatakia kila la kheri na nitawakilishwa na Mkuu wa Wilaya  ya Tanga Mheshimiwa Halima Dendegu”Alisema Mh. Gallawa
  Chini  ya utaratibu huo Vodacom Tanzania pia itafuturisha watoto yatima na  wa-Madrasa katika miji mbalimbali nchini sanjari na utoaji wa sadaka za  vyakula na vifaa vya shule kwa watoto hao.