Pages

Saturday, July 28, 2012

*RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA HANGA LA PRECISION AIR DAR ES SALAAM

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi hanga la Precisionair katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi.Kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Precision air Bwana Michael Shirima.

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege la Precision Air Bw. Michael Shirima akimkabidhi zawadi Mh Rais Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuzinduz rasmi karakana na ndege za shirika hili (Hanga) kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo jijini Dar es salaam, Karakana hiyo itakuwa na ikihudumia ndege za shirika hilo la mashirika mengine pia lakini pia itapokea wanafunzi walio kwenye mafunzo ya Uinjini wa ndege kutoka katika vuo vya ndani.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe pamoja na wakuu mbalimbali wa shirika la ndege la Precision Air na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada ya uzinduzi wa (Hanga) hiyo
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Alfonce Kioko alipokuwa akitoa maelezo wakati wakati Rais alipokuwa akikagua Hanga hiyo, kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe.

Popular Posts