Pages

Thursday, July 26, 2012

KUKABIDHI NYARAKA ZA KIUTENDAJI, TAWI LA CCM MOSCOW

Yah: KUKABIDHI NYARAKA ZA KIUTENDAJI, TAWI LA CCM MOSCOW- 24 July 2012
Nakujulisha;
Baada ya kuhitimu masomo ya chuo nchini Urusi na kuhitajika Tanzania kwa utendaji Majukumu ya kitaaluma:
Na kwa kuzingatia dhamana , heshima na ushirikiano mkubwa toka kwa sekratarietiya ya tawi na viongozi wa kamati za tawi ,baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya katibu wa tawi kuanzia June 2011, nafasi iliyoachwa wazi kufatia kurejea nyumbani kwa Assenga Boniface aliyekuwa katibu wa tawi.
Hivyo basi ,kwa mamlaka ya mwongozo wa tawi la CCM Moscow, nawajulisha kuwa leo siku ya Jumanne , tarehe 24 July 2012, katika kikao maalum kilichoitishwa cha makabidhiano ya nyaraka za tawi kulingana na utekelezaji wa majukumu ya kiutendaji. Viongozi wafutato walialikwa kuhudhulia makabidhiano:

1. Ndg Kassim Kolowa (katibu Mwenezi na sera , Tawi)
2. Ndg Salim Mfungahema (Naibu -Katibu Mwenezi na Sera, Tawi)
3. Bi Rehema Simba.(Mwenyekiti , UWT- Tawi)
4. Bi Hilda Kifanga (Katibu , fedha na Uchumi-Tawi)
5. Ndg. Manda Shabani (Mjumbe kamati ya maadili)
6. Ndg. Azizi Chuma (Mjumbe wa Halmashauri kuu)
7. Ndg. Octavian Nyalali( Katibu, UVCCM -Tawi)

Baada ya Maelezo mafupi ya Utangulizi kuhusu tawi la CCM Moscow na mwelekeo wake toka kwa Bwana Bakunda , ilifuata taarifa kuwasilishwa mezani juu ya Kiongozi atakaye kuwa na wajibu wa kukaimu Utendaji Mkuu wa Tawi la CCM Moscow ( Acting General Secretary), Kufuatia Kuhitimu Masomo kwa aliyekaimu nafasi hiyo Ndg Bakunda Chrispin, ambaye sasa anarejea Tanzania ili kutimiza majukumu mengine ya kitaaluma aliyosomea.(Teknolojia ya Mafuta na Gesi)

Kwa Kuzingatia "maelekezo" ya Mwenyekiti wa Tawi ambaye ana Mamlaka kimwongozo ya Uteuzi wa nafasi ya kiongozi yeyote wa tawi , Mwenyekiti wa Tawi la CCM Moscow , Dr.Afred Kamuzora amemteua Ndg KASSIM KOLOWA kuwa KAIMU KATIBU WA TAWI LA CCM MOSCOW.

Ndg KASSIM KOLOWA anawajibika na kuwa dhamana ya UTENDAJI MKUU WA TAWI LA CCM MOSCOW MPAKA HAPO ITAKAPOTANGAZWA VINGENEVYO.
Aidha Bwana SALIM MFUNGAHEMA atakuwa katibu kamili wa maswala ya sera na uenezi wa Tawi. Nafasi zingine za Uongozi wa tawi zitabaki kama zilivyo.

Imetolewa na -
Idara ya Mawasiliano-Tawi la CCM Moscow. 24 July 2012

Popular Posts