Pages

Wednesday, July 25, 2012

Mzee CUF

Huyu ni Mzee CUF, ni maarufu kwa upigaji picha za kuuza 'BANYAA' huyu pia ni miongoni mwa wapiganaji ambao walipata kupigania haki ya Mtanzania wa leo enzi hizo, ambaye kwa sasa kazi yake kubwa ni kujishughulisha na uuzaji wa picha katika shughuli mbalimbali, hapa akihaha kusaka matukio ya kuweka katika karatasi ya picha zake ambazo baadaye atafanya biashara. Mzee huyu baada ya kuona siku ya leo ni muhimu hata kwake pia lakini akiweka kazi yake mbele zaidi ili kujipatika kipato alionelea ni vyema naye pia akakumbukia mavazi yake haya aliyoyavaa na kutinga nayo eneo la tukio ili kuepuka kusumbuliwa na wahusika aweze kuingia kirahisi eneo la tukio kama unavyomuona akiwa bize na vazi lake huku akiwa na begi kubwa la kamera wakati kajikamera alikonako ni kibiriti. Hii yote ni janja tu ilimradi mkono uende kimiani.
Mzee CUF, akiwa bize kunasa picha za wajeda wakiwa katika paredi, begani ni bonge la begi la kamera ambalo ndani yake halina kilichokusudwa.
Mzee CUF bado yu bize........

Popular Posts