Mratibu wa Coconut Fm Ali Khatib Dai  (kushoto) akimkabidhi rambirambi makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000/-)  ofisini kwake Vuga mapema leo
   Meneja wa Coconut Fm Husna Abdul  akisalimiana na Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar walipokwenda kukabidhi rambirambi  kufuatia ajali ya meli ya MV Skagik.
   Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akitoa maelezo kwa mratibu wa Coconut Fm Ali Khatib  Dai kuhusiana na hali inayoendelea kuhusiana na ajali ya kuzama kwa  meli ya MV Skagik Prime Time Promotion kupitia kituo chake cha redio  Coconut Fm kimekabidhi rambirambi ya kiasi cha shilingi milioni moja  (1,000,000/-) kwa makamu wa pili wa raisi wa Zanzibar Balozi Seif Ali  Iddi kufuatia na kuguswa kwake ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagik.