Rais  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi  Afande Saidi Mwema, na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange,  baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini  Dar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walikokwenda  kuhudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo. 
Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, wakiwasili Uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni  wakitokea Burundi na Rwanda walikohudhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru  wa nchi hizo. Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe  Saidi Mecky Sadik. PICHA NA IKULU

