Bondia  Japhet Kaseba akipima uzito.
   Francis Cheka nae akipima uzito wake.
  Mabondia hao wakitunishiana misuli.
   ...Wakiwa tayari kwa mpambano wa kesho. 
  Cheka akipimwa mapigo yake ya moyo.
  ...Kaseba nae akipimwa.
  ---
  Mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba  leo wamepima uzito wao tayari kwa mpambano wa kesho katika Tamasha la  Matumaini litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  Mabondia hao wamepima uzito wao katika hoteli ya The Atrium iliyopo  Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam ambapo kila mmoja amemtambia  mwenzake kuwa ataibuka kidedea katika pambano hilo.