Mwananchi  wa Kijiji cha Muyuni Shukuru Ramadhani akitoa maoni yake  kuhusu katiba  mpya huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
   Mwenyekiti  wa Ukusanyaji maoni ya Katiba Mpya Mohd Yussuf Mshamba  akifahamisha  namna ya utoaji wa maoni unavyotakiwa huko katika kijiji  cha Muyuni  Mkoa wa Kusini Unguja.
   Wajumbe wa kukusanya maoni ya Katiba mpya wakiandika maoni ya wananchi huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
   Mwananchi  wa Kijiji cha Muyuni Mwanapili Haji Mussa akipeleka maoni yake  kwa  njia ya Barua yanayohusu uundwaji wa katiba Mpya kwa wajumbe wa   Ukusanyaji maoni hayo huko Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
   Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika utoaji wa Maoni huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
   Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika utoaji wa Maoni huko katika Kijiji cha Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
  -- 
   TUME   ya taifa ya kukusanya maoni juu ya marekebisho ya Katiba inaendelea   kukusanya maoni katika mkoa wa Kusini Unguja kwa wananchi mbalimbali   ambapo inapokea maoni mbalimbali pamoja na kero za wananchi.
  Wakitoa  maoni  yao kwa Tume hiyo wananchi wa Muyuni huko skuli ya Muyuni B  wananchi  hao wamesema wanataka kuwepo kwa mfumo utaweza kuondoa kezo  zilizomo  katika muungano ambazo ni changamoto kubwa  kwa wazanzibar. 
  Aidha  walisema  wanataka kuwepo na serikali ya Zanzibar ambayo itakuwa na rais  wake  ambae anatambulika kitaifa na kimataifa , kuwepo na serikali ya   Tanganyika na rais wake pamoja na serikali ya muungano ambayo itakuwa ya   mkataba 
  Wananchi hao waliitaka tume hiyo kuwepo na usawa katika serikali zote mbili zikiwemo mafuta, madaraka pamoja na utawala.
  “Tunataka   usawa na haki katika serikali zote mbili ambapo sisi wanzanzibar   hatupati kitu katika muungano tunaomba marekebisho katika mafuta,   madaraka na utawala”, walieleza wananchi hao.
  Aidha  baadhi  ya wananchi hao wameitaka kuwepo na mfumo tofauti wa kielimu,  kisarafu,  kiulinzi pamoja na vyanzo vya mapato ili Zanzibar iweze  kujitegemea  wenyewe kimapato na kimaendeleo.
  Hata  hivyo  wananchi hao waliiambia tume hiyo wanataka ZanzĂbar iwe na  mamlaka yake  kamili na isiingiliwe katika maamuzi yake inayojipangia  kama zilivyo  nchi nyengine.
  “Zanzibar   haijapata mamlaka yake kamili tunataka tuwe na mamlaka ambapo tunataka   isiingiliwe katika maamuzi yake wanachoamua wazanzibar kiwe hicho hicho   kisibadilishwe”, walifafanua wananchi hao.
  Baadhi  wa  wananchi hao walitaka kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu ambapo  kutaweza  kuwepo kwa usawa na mamlaka ya nchi pamoja na utawala wake na  wengine  walitaka kuwepo na marekebisho ya katika pamoja na kero za  muungano.  
  Na
  Miza Kona 
  Maelezo Zanzibar