
  Pichani  Juu  Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula  kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto  yatima wa kituo cha Maunga Centre.
 
 Pichani Juu na Chini  ni Wanafamilia wa  Jay Dee wakipakia mizigo tayari kuelekea kituo cha kulelea watoto yatima  cha Maunga Centre kwa ajili ya kukabidhi msaada.
 
  
 Baadhi ya wanafamilia katika pozi kabla ya kuanza safari ya kuelekea kituo cha watoto yatima cha  Maunga Centre.
 
 Kiongozi wa msafara LadyJay Dee akielekea kupanda usafiri maalum ulioandaliwa.
 
 Wanafamilia ndani ya basi kuelekea Maunga Cente kituo cha watoto yatima kwa shughuli nzima ya kukabidhi msaada.
 
 Wanafamilia Ester Ulaya Cathbert na  Maggie wakifanya shopping katika maduka ya Kinondoni njiani kuelekea  kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.
 
 Judith G. Habash a.k.a Komando Binti  Machozi Lady Jay Dee akiwasili na Familia yake katika Kituo cha kulelea  watoto yatima  cha Maunga Centre kilichopo maeneo ya  Kinondoni  Hananasifu.
 
 Wanafamilia wa Jay Dee wakishuka kwenye basi baada ya kuwasili.
 
 Vijana wa Familia ya Jay Dee wakishusha  msosi ulioandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya watoto yatima wa Kituo  cha Maunga Centre.
 
 Baadhi ya zawadi zilizopekwa na Jay Dee Family katika kituo cha kuelea watoto yatima cha Maunga Centre.
 
 Mwanafamilia wa Jaydee Wise Monica Kaaya akionyesha Upendo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
 
 Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi. Zainabu Bakari akionyesha chumba wanacholala watoto wa kiume katika kituo hicho.
 
 Hiki ni chumba wa wasichana.
 
 Hapa ni mahali wanapotundikia neti.
 
 Hiki ni choo wanachotumia yatima hao ambacho hakijaezekwa na bati.
 
 Sehemu wanatotumia kupikia chakula.
 
 Mtoto Khadija Mussa akisoma Risala kwa  mgeni rasmi Komando Lady Jay Dee na Familia yake (hawapo pichani) ambapo  amezungumzia changamoto ya mahali wanapoishi haparidhishi na kuwataka  wadau kujitokeza kuwasaidia kuboresha eneo lao ikiwemo Choo, Sehemu ya  kulala pamoja na ada za twisheni kwa watoto hao.
 
 Wanafamilia wakisikiliza risala ya Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
 
 Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo pichani).
 
 Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
 
 Lady  Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele,  Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na  vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho  Bi.  Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika  kituo hicho Khadija Mussa.Jay  Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango  chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi  wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
 
 Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
 
 Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto) akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay Dee.
 

 Pichani  Juu Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula  kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto  yatima wa kituo cha Maunga Centre.
 
 Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
 
 Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
 
 Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi  Zainabu  Bakari ambapo amezungumzia changamoto zinazowakabili ni sehemu  ya kuishi wahudumu wa kituo hicho, mishahara ya kuwalipa wahudumu na  makazi ya wahudumu wa kituo hicho.Bi. Zuhuru Bakari alisema kituo hicho  kinalea watoto 30 ambapo watoto 20 wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya  walezi waliowachagua wao kutokana na ufinyu wa eneo jumla yake  inatengeneza idadi ya watoto 50.
 
 Mwanafamilia Ester Ulaya akizungumza kwa  niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema watakuwa bega kwa bega na kituo  hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili wa kusaidia kituo hicho.
 
 Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
   Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.
 
 Zainul Mzige wa MO BLOG alijumuika na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
 
 Wanafamilia wa Jay Dee katika picha ya  pamoja baada ya kuhitimisha zoezi zima la kutoa msaada kwa kituo cha  watoto yatima cha Maunga Centre.
 