Mmoja  wa majaji wa shindano la  Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika  kwenye Club ya Mawingu jioni ya leo,jijini Arusha ,Hamis Mandi a.k.a B  Dozen kutoka kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds  FM,akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi shindi la  shindano hilo liitwalo Contagious Crew
  Baadhi  ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya SBL,wakimkabidhi mmoja wa wacheza  shoo wa kundi la News Contagious Crew kreti la bia ya Serebgeti,mara  baada ya kuibuka washindi wa shindano la  Serengeti Dance la Fiesta  2012,washindi wa pili walikuwa ni kundi la New Kings ambao wao  walijinyakulia kreti la bia.
  Mwendesha  shindano hilo pichani kati,Nikson akisoma majina ya makundi mawili  yaliyoingia fainali na hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa  na kundi la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha  shilingi milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengeti,ambao  ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.
  Pichani  majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakijadiliana  jambo wakati wa mchuano mkali wa shindano hilo lililokutanisha makundi  manne,ambayo ni Tp Jackson,New Kings,B-Boy Dance pamoja na kundi la  Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami kutoka THT na shoto ni Mtangazaji  kutoka Clouds TV,Issa Kwisa
  Kundi  la Tp Jackson  likifanya vitu vyake jioni ya leo wakati wa shindano  la Serengeti Dance la Fiesta 2012 likiendelea,Katika shindano hilo kundi  la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi  milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengei,ambao ndio  wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.
  Sehemu ya washabiki wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakivutiwa zaidi na shindano hilo lilipokuwa likiendelea ukumbini humo.
  Kila kundi lilionesha umahiri wake wa kucheza,huku kwa aliyeonekana kufanya vyema shangwe na miluzi ilitawala kila kona.
  Palikuwa  hapatoshi jioni ya leo ndani ya Club ya Mawingu wakati wa shindano  la Serengeti Dance la Fiesta 2012 likifanyika,ambapo kila kundi  lilionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma kwa staili ya kipekee  kabisa.Pichani mcheza shoo wa kundi la B-Boy Dance akionesha umahiri  wake wa kucheza.
  Vijana  mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye shindano la Serengeti Dance  la Fiesta 2012,ambapo mshindi alifanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi  milioni moja na kreti moja la bia mshindi wa pili aliibuka na kreti la  bia ya serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kwa mwaka  huu.
  Pichani  kati mmoja wa majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012  akizungumza machache wakati wa mchuano mkali wa shindano hilo  lilikutanisha makundi manne,ambayo ni Tp Jackson,New Kings,B-Boy Dance  pamoja na kundi la Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami kutoka THT na  shoto ni Mtangazaji kutoka Clouds TV,Issa Kwisa
  Waratibu  wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 na Mc Shujaa jijini Arusha,ambao pia  ni watangazaji kutoka Clouds FM, Ruben Ndege a.k.a Ncha Kali na Adam  Mchomvu a.k.a Baba Jonii wakifuatilia kwa makini shindano la Serengeti  Dance la Fiesta 2012 lililofanyika jioni ya leo ndani ya ukumbi wa  maraha wa Mawingu,jijini Arusha.
 









