Pages

Tuesday, July 3, 2012

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ilivyoanza Kazi Mkoa wa Kusini Unguja, Katika Vijiji vya Mzuri na Mtende

Mwananchi wa kijiji cha Mzuri Makunduchi Bakari Ubwa, akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ametaka kuwe na Serekali mbili ya Zanzibar na Tanzania Bara na kila Serekali iwe na uwezo wake na Rais wa Zanzibar awe na uwezo wa kuamua mambo yake kwa ajili ya Zanzibar,Rais wa Zanzibar awe na uwezo wa kuchagua Mabalozi kwa ajili ya Zanzibar na Rais wa Tanzania pia na yeye achaguwe mabalozi wa Tanzania.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Balozi Salim Ahmed Salim, akizungumza kuhusiana na utoaji wa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mtende.
Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, akisoma vipengele wakati wa kutowa maoni ya mabadiliko ya katiba katika viwanja vya Mtende Makunduchi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania Dk Mvungi, akitowa maelezo kwa Wananchi wa Kijiji cha Mtende waliofika kutoa maoni yao katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania wakifuatilia maoni ya Wananchi wa Kijiji cha Mzuri wakiyatowa mbele ya Tume hiyo ilioanza kazi yake jana katika Wilaya ya Kusini Unguja Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi akikabidhi barua yenye maoni yake kuhusu Mabadiliko ya Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya mpira timu ya Mwenge Mzuri,
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua yake yenye maoni yake kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume hiyo ilipofika katika Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Ali Khamis Ali, akichangia maoni yake kwa kuanza kwa historia kuhusu Mzee Karume, ambaye amesema Unguja itakuwa kama peponi na kweli ilikuwa hivyo kwa kujenga Nyumba za Wazee Sebleni na kuanzisha Viwanda mbalimbali katika Zanzibar.Amesema kuwepo kwa serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika na kutaka kuwe na Muungano wa Mkataba na kugawana sawa kwa sawa misaada inayopatikana. na mambo ya muungano kugaiwa sawa.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Duli Ali Duli, akichangia maoni yake kwa Tume iliofika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, amesema kuwe na Serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika, na kuondoa kasoro zilioko katika Muungano huu.
Mwananchi wa Mtende Abuu Kombo Ramadhani, ametowa maoni yake kuwe na serekali mbili na kuwe na uwiano katika nafasi za Muungano kwa pande mbili hizi na Zanzibar iwe na rasilimali zake wenyewe bila kuingiliwa na upande mwengine. na bara iwe hivyohivyo.
Mwnchi wa Kijiji cha Mtende Mohammed Shaka Mussa, amesema nashukuru kuitwa Tanzania na pia Umoja ni Nguvu,Utengano ni Udhaifu. Amesema kuwepo na serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika na kila upande uwe na uwezo wa kuamua mambo yake na kuondoa kasoro za Muungano zilizopo ili kuimarisha umoja wetu.
Wananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi wakiwa katika viwanja vya Mwenge wakishiriki kutowa maoni yao wakisikiliza maoni ya Wananchi mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania.iliyofika katika kijiji hicho kukusanya maoni ya Wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Mtende wakisikiliza maoni yanayotolewa na Wananchi wa Mtende mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba katika viwanja vya skuli ya Mtende
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania Balozi Salim Ahmed Salim. akibadilishana mawazo na Wazee wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja, baada ya kumalizika kwa utowaji wa maoni kwa Wananchi wa Kijiji hicho.Picha Zote na Mdau Mapara Othman-Kusini Unguja

Popular Posts