Gari la Fusso lililo sababisha Ajali hiyo 
 Namba za gari la Fusso
 Toyota Rav 4 ikiwa imebamizwa vibaya na Fusso hilo 
 Gari la Rav 4 lilivyo haribika kwa nyuma
 Namba za Gari la Rav 4
 Fusso kwa nyuma 
 Fusso kwa Mbele 
***********************************
Ajali Mbaya imetokea usiku huu iiyo husisha Gari la Fusso namba T 596 BUB pamoja na Rav 4 namba 
T 675 ATK, Maeneo ya CCM Mkoani Mbeya. 
Shahidi  aliye kuwepo eneo la tukio amedai  ya kuwa Dereva wa Gari la mizigo  Fusso alikuwa mwendo kasi sana, na huku akijaribu kuyapita magari  mengine matano ambayo yalikuwa mbele yake. Wakati huo anaendelea  kuyapita magari hayo tayali dereva wa Rav 4 alikuwa amesha washa taa  kuonesha kuwa anaelekea kulia na ndipo Dereva wa fusso akaligonga Gari  la Rav 4 ambalo baada ya hapo liliseleleka kwa umbali wa Takribani mita  300 kutoka usawa wa sehemu ambapo liligongewa. 
Hata hivyo dereva wa Fusso aliyesababisha Ajali hiyo amekimbia eneo hilo. Hakuna aliye umia wala kupata majeruhi.
http://mbeyayetu.blogspot.com/
http://mbeyayetu.blogspot.com/






