Mkurugenzi  wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi  mfano wa  hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi  wa  harambee hiyo.kushoto meneja rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
 Mgeni  rasmi wa harambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa  kampuni ya  Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma  baada ya  kuchangia sh. milioni 22.
Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja   (katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya   kuchangia sh. 500,000.
 Meya  wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa   hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward   Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa   elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo   zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400   zilipatikana.
 .Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Wadau  mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo,wakiongozwa na Waziri Mstaafu  Edward Lowassa(wa Pili Kulia) na Meya Wa Ilala Jerry Silaa 
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Mbunge  wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa  Manispaa  ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya  kuchangia  mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata  hiyo Bonah  Kaluwa,  wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa  mgeni  rasmi kuingia ukumbini.Picha Zote na Dotto Mwaibale
---
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.
---
  WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa  mbele  katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya   kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya   Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam. 
  Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo  juzi  katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam   ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10. 
  Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa   ni  Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22,  African  Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line   ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja   alichangia milioni Sh.10. 
  Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,   Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds   walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh.   milioni 12.
  Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka   Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha   wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu. 
  Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa  jitihada  zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani  wengine  kuiga mfano huo. 
  Diwani wa Kata ya Kipawa,  Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule   saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo   lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha   wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja. 
.  “Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi,  kwa  mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane   wakati wanafunzi waliopo ni 2,200,  Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu   madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa. 
  Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa   ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa   matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 
  Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15  kilichangwa na wadau  mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3  zilitolewa na Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group  ambao walitoa shilingi milioni  moja na wanafunzi kadhaa wa shule za  msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali.