Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, wachapishaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Sunday News na HabariLeo, Bw. Mkumbwa Ally 
Mpiganaji Athumani Hamisi akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam juzi
---
Tarehe  5 Juni,2012, mfanyakazi waKampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ambaye  amelemaa baada ya kupata ajali yagari, Bwana Athumani Hamisi, aliitisha  mkutano wa waandishi wa habari kwenyeukumbi wa Maelezo, Dar es Salaam,  na kutoa taarifa iliyojenga taswira kuwaametelekezwa na TSN pamoja na  Serikali.
TSN inapenda kufafanua kuwa Serikalina kampuni hii, ambayo ilimwajiri Athumani tarehe 1/09/2006 kama Mpiga pichaMwandamizi, wamemhudumia mfanyakazi huyo kikamilifu tangu alipopata ajalitarehe 12 Septemba, 2008 hadi sasa, na huduma hiyo inaendelea.
Baada ya kutokea ajali hiyo, TSN kama mwajiri ilisimamia matibabu yake ya awali katikahospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI) mpaka Serikali, kwakupitia Wizara ya Afya ilipomhamishia Netcare Rehabilitation Hospital nchini AfrikaKusini kwa matibabu zaidi.
 
Serikali  ililipia gharama za matibabuyake yote akiwa Afrika Kusini kwa kipindi  cha mwaka mmoja na miezi saba, ambayoyanazidi shilingi milioni mia  moja.Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa kigari maalum ambacho Athumani  anatumiasasa.
TSN kama mwajiri ililipa nauli yandege kwenda na kurudi pamoja na posho ya kujikimu ya mgonjwa pamoja na nduguwasindikizaji ambao ni Bw. Hassan Hussein na Bi. Mirriam Malaquias.Posho yakujikimu ilikuwa USD 6,210 sawa na Shilingi 9,315,000, na nauli kwa watu watatu ilikuwa ni Shilingi3,535,869.92. Athumani aliendelea kupatiwa huduma akiwa huko Afrika Kusini kwagharama za Serikali na TSN mpaka aliporejea nchini tarehe 08/05/2010. Gharamazilizolipwa na kampuni kwa mfanyakazi huyu hadi sasa ni takriban shilingi million 52.
Athumani aliporejea nchini alilakiwana wafanyakazi na viongozi wa TSN na kupangiwa chumba hoteli ya Holiday Inn wakatiutaratibu wa kumtafutia nyumba ya kupanga ukikamilishwa. Kampuni ilitumia kiasicha Shilingi 1,756,979.50 kulipia hoteli. Baadaye alipelekwa kwenye nyumbaambayo alipangiwa na Kampuni katika eneo la Sinza Vatican ambapo ndipo badoanaishi hadi hivi sasa. Gharama ya nyumba kwa mwaka wa kwanza 2010 ilikuwa niShilingi 4,200,000 au Shilingi 350,000 kwa mwezi. Mwaka 201 mwenye nyumba alipandisha kodi hadi400,000 kwa mwezi ambapo Kampuni ililipia Shilingi 4,800,000. Kodi hiyoimeishia Mei mwaka huu na kampuni imeshafanya mazungumzo na mwenye nyumba iliAthumani aendelee kuishi hapo kwa muda wakati mipango endelevu ya ustawi wakeinafanywa kwa kuzingatia taratibu za ajira.
Mnamo tarehe 8/12/2010 Athumanialirudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake namatibabu yaligharimiwa na Serikali wakati TSN iligharamia nauli yake na yamuuguzi wake, pamoja na posho ya kujikimu Shilingi 6,300,000/-.
Pamoja na bwana Athumumai kulalakitandani kwa muda wote huo ameendelea kulipwa mshahara kamili bila kukatwakama mfanyakazi wa kawaida ikiwa ni msaada wa kampuni kwa kuzingatia ulemavualioupata.Mshahara aliolipwa kwa muda wote aliokuwa anaugua ni kiasi chashilingi 26,773,000. Vile vile kampuni ilimlipa muuguzi toka Afrika Kusiniambaye alikuwa anamhudumiaa Athumani Rand 12,500 kama mshahara wake.
Kuanzia Januari 2011, mshahara waAthumani umejumuisha asilimia 15 kama posho ya nyumba ambayo wafanyakazi wotewanalipwa. Aidha Athumani yupo kwenyempango wa bima ya afya anayolipiwa na kampuni, ambayo inamwezesha yeye nafamilia yake kuweza kutibiwa katika hospitali yoyote hapa Tanzania. Kampuni inamlipia Shilingi 68,449.20 kilamwezi na bima hiyo ndiyo inayogharamia matibabu yake yote hapa nchini.
 
Bwana  Athumani anapatiwa usafiri naTSN mara mbili kwa wiki kumtoa nyumbani  hadi Muhimbili na kurudi kwa ajili yamazoezi ya viungo. 
Imetolewa na
OFISI YA MHARIRI MTENDAJI
08.6.2012
OFISI YA MHARIRI MTENDAJI
08.6.2012
------
*Chini ni Nakala ya Maombi ya Mpiganaji Athumani Hamisi Aliyoitoa Kwa Waandishi Wa Habari Jijini Dar es Salaam Juzi
---
Mimi Athumani Hamisi
Awali ya yote, napenda kuwasalimia wote, wakubwa na vijana wenzangu
Hii  itakuwa mara ya pili kuongea nanyi waandishi wenzangu, ndani ya miaka  minne tokea nipate ajali Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani  nikiwa na wenzangu Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu na Anthony  Siyame, tukiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi  kikazi. Mara ya kwanza  niliongea nanyi 2010 baada ya kurejea kutoka Afrika kusini nilikopelekwa  na Serikali kwa matibabu.
Shukrani  zangu za awali, zimwendee Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya Kikwete aliyenitembelea katika Hospitali ya Muhimbili nilikolazwa  na kuagiza nilipelekwe nje kwa matibabu zaidi.
Katika  ajali ile, nilivunjika shingo na ku-damage spinal cord iliyopelekea  kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Katika operesheni iliyofanywa na  madaktari wa hospitali ya Mil Park, Afrika Kusini walilazimika  kuunganisha shingo kwa nyuma.
Shukrani  za pili ni kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni  ninayofanyia  kazi ya magazeti ya serikali, wachapishaji wa Daily News, Sunday news,  Habari Leo Jumapili na Spoti leo, familia yangu iliyokuwa katika wakati  mgumu wakati huo hadi sasa watanzania wote wuamini wa dini zote  waliokuwa wakiombea Pamoja na marafiki zangu waliokuwa wakihangaika huku  na kule kwa namna moja ama nyingine .
Niko mbele yenu leo kuwaomba mnifikishie ujumbe kwa jamii kwa maelezo yafuatayo:-
- Ofisi yangu ya TSN ilinipangia nyumba ninayokaa Sinza Vatican, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mei 2010-2011 na mkataba ulikukwa kati ya mwenye nyumba na TSN ambao mimi sikuwahi kuuona hadi ninavyoongea na nyie leo.
 
- Mkataba uliisha tena Mei 2011, mwenye nyumba alikwenda TSN kuomba kusaini mkataba mpya. Badala yake aliandikiwa mkataba mpya wenye jina langu na kupewa aniletee mimi nisaini. Nilipomuuliza mkataba wa kwanza uliingia na nani na ni nani alisaini. Alisema ni TSN walisaini wakamwambia wana mgonjwa ambaye ni Staff wake atakuja kuishi pale akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu. Mwenye nyumba akasema walimwambia gharama za nyumba ni za TSN , sasa nashangaa leo wameandika jina lako na mkataba ni kati yangu na wewe.
 
- Nikamwambia kaka, mimi sikutarajia kufikia hapa kwani mwaka 1999 ilipangwa mimi nifikie katika nyumba ya kampuni Upanga kuepusha gharama na ukaribu wa huduma za kitabibu, mpaka masuala yangu yatakapothibitishwa na Daktrari kama hali yangu itaruhusu mimi kuweza kufanyakazi ama vinginevyo. Rudi ofisini mkasaini kama mlivyofanya awali. Na umwambie kwa hali ya Athumani hawezi kusaini mkataba na mimi kulingana na hali yake. Isitoshe mi nilitiliana saini mkataba wa awali na TSN.
 
- Ukweli nilikataa kusaini zaidi ya mara tatu, mpaka Meneja Mwajiri siyo huyo wa sasa alipoingilia kati na kunithibitishia kuwa kampuni italipa nyumba mpaka uamuzi wa madaktari utakapotoka, saini mimi nitakulinda. Niliporejea nyumbani nikawekwa wino katika dole gumba wakaweka saini. Mpaka yalipojitokeza ya sasa.
 
- Ndugu waandishi wa habari, hali yangu japo imeimarika zaidi kuliko awali, leo nimekuja na jambo ambalo litahusisha jamii na nyie ndiye wahusika wakuu katika suala hili.
 
KIKUBWA ZAIDI LEO NI SHUKRANI NA OMBI
Ukweli  ulio wazi, nashukuru  kwa Mungu na kujivunia kuwa TSN . nimelelewa na  TSN kwa miaka sita sasa. Imenilea nikiwa mgonjwa kwa miaka mine, nikiwa  bado niko ndani ya ajira jambo ambalo ni gumu sana sehemu nyingine.
Imelipa  nyumba kwa miaka miwili na imesitisha kulipa kodi ya 2012-2013 kwa   barua ya Februari 3,2012 na kutoa maelezo kwenye barua kuwa imefikia  hatua hiyo kutokana na kuwapa wafanyakazi wake asilimia 15 ya mishahara  yao kulipa nyumba. Nyumba walionipangia ni ya vyumba viwili na kodi  iliyolipwa kwenye mkataba wa mwaka jana ni Milioni 4.8
Nilipatwa  na mshutuko kidogo, nafsi ikanishauri niite menejiment nyumbani  tushauriane katika hili. Walikuja Machi 28, na wakanipa pole ya kampuni  tokea nirudi 2010 Shs 50,000. Lakini mazungumzo hayakuisha kutokana na  muda na kuahidi kurudi wiki inayofuata kwa mazungumzo zaidi. Nimepewa  notisi na mwenye nyumba April 23,2010.
Nadhani  kutokana na kubanwa na kazi, hawakupata nafasi ya kurudi tena kumalizia  mazungumzo. Kwa mtazamo wa kifikira ni wazi msimamo ulibaki palepale.  Barua ya kusitisha kulipa kodi haikuja kwangu tu bali pia mwenye nyumba  alipata.
UFAFANUZI
Kabla  ya kuruhusiwa kurejea nyumbani Tanzania, Netcare Rehabilitation  Hospital, wanautaratibu mzuri sana. Kabla ya kuwa –discharged  wanakuruhusu ukae nje ya hospital kwa miezi mitatu, kama una mke au mume  na kama huna utatafutiwa nurse awe wa kike ama wa kiume mimi nilipata  nurse. Baada ya hapo una hudhuria mazoezi na vipimo kadhaa kwa miezi  mitatu. Ukifaulu kumaliza miezi mitatu wewe na mwangalizi wako hasa wewe  mgonjwa bila kupata matatizo, hapo wanaku-discharge.
Nilipiga  simu kwa Katibu Kiongozi Ikulu wakati huo, Philemon Luhanjo na kwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii anahitajika nurse kuja  kukaa nami nje ya hospital kwa miezi mitatu, je mtanisaidiaje? Kwa kweli  jibu lao lilikuwa moja tu hatutatuma nurse kutoka huku, tafuta huko  huko, fedha za kumlipa, nyumba ya kulala, chakula na usafiri, andika   budget itume haraka tutalipa na wasiliana na ubalozi waje kujua unakaa  wapi  na fedha zitatumwa ubalozini watakuwa wanakuletea.
Nilipata  nurse na miezi mitatu ilipokaribia kwisha nilifanya mawasiliano kujua  kama kutatumwa mtu wa kunifuata, wakanijibu njoo naye huyo huyo  watanzania waliofanikiwa kuangalia vyombo vya habari wengi walimuona  kwani nilirudi Mei 28, 2010. Baada ya mwezi alimaliza mkataba name  kutakiwa kutafuta nurse wa kukaa naye kwa saa 24 . akapatikana na  akafundishwa na M-South Africa jinsi ya kukaa na mgonjwa wa Spinal Cord.
TSN,  wakamlipa nurse wa South Africa Rand 12,500 alizokuwa anadai na  palepale nikauliza vipi  kuhusu malipo ya nurse mpya ambaye ataachwa na  mimi? Kwa sababu serikali imemaliza jukumu lake na waliniambia kwa kuwa  wewe bado ni mwajiriwa wa TSN, jukumu lote sasa utakuwa chini yao na  ndiyo mmepewa pia jukumu la kumlipa kama mlivyofanya leo. TSN walinijibu  palepalekuwa suala la kumlipa nurse ni lako na familia yako ila nyumba  tutalipa.
Vodacom walijitokeza kubeba gharama za tiketi nilipopata ajali kwenda Afrika Kusini na wasindikiaji wote, tiketi ya nurse niliyekuja naye. Pia wakalipa tiketi yangu na nurse Desemba 8,2010 kwenda na kurudi Afrika Kusini kwa ajili ya checkup.
Baada  ya TSN kulipa nurse yule msouth afrika, nikawapigia Vodacom Foundation  kuwa nurse amemaliza mkataba na ameshalipwa fedha naomba mumkatie  tiketi. Hivyo  ilikuwa Juni 25 na kesho yake Juni 26 2010 jioni wakaja  watu wawili kutoka Vodacom Foundation na mmoja kutoka TSN waliniambia  wamekuja na vitu vitatu.
- Wakamshukuru nurse kwa kazi nzuri , lakini wakamwambia , sisi ni kutoka Vodacom. Vodacom Foundation inakuomba uendelee kumhudumia Athumani . Na Vodacom watakulipa mshahara lakina tunaomba upunguze kiwango.
 
- Yule nurse akakubali akapunguza nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa na serikali. Wakamwambia sasa Vodacom Foundation inakata tiketi ya kwenda nyumbani Afrika kusini kuaga. Akaomba siku 15, mkataba wa mdomo ukakubaliwa na yule nurse na mshahara wa kwanza ukawa Julai 2010 kuendelea na kazi chini ya Vodacom. Julai 2010 wakamlipa. Kilichoendela naomba nisiseme.
 
- Muda wa checkup ulifika Desemba 2010, nikaitaarifu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Wakakubali wakaandika barua kwa kugawa majukumu. Afya wakasema watalipa gharama za matibabu, Vodacom tiketi za kwenda na kurudi na TSN waliagizwa kulipa allowance kwa mgonjwa na nurse. Tukasafiri Desemba 8,2010 na tukarudi Februari 28,2011. Malipo yaliyofanywa na TSN kidogo ni aibu naomba nisiseme.
 
- Hali hiyo ilinionyesha kuwa Vodacom Foundation walikuwa wanatambua uwepo wa yule nurse. Lakini hadi nurse anaondoka alilipwa mshahara mmoja tu na hata tiketi ya nurse kurudi Afrika Kusini Vodacom hawakulipa.
 
- Nililipa tiketi ya Business Class. Nikampa Rand 4,500 akakataa akachukua Rand 2,500 tu , akaniambia, Athumani nakuacha katika hali mbaya sana. Fuatilia haki zangu na zako, ukifanikiwa utaniambia na Account ya benki , First bank nakuachia utaniwekea. Vodacom Foundation hawajawahi kupokea simu yangu na Mkurugenzi wake hajawahi kupokea simu yangu wala kuongea na mimi tokea nipate ajali.
 
- Suala lingine waliniuliza nichague kitu kimoja, kujengewa nyumba au kusomeshewa watoto. Mimi nilichagua kujengewa nyumba. Walichukua chaguo langu. Tukamaliza mazungumzo.
 
- Baada ya mwezi waliniambia suala lako limekubaliwa ila tumepata Mkurugenzi mpya, lakini usijali. Mpaka hapa ninavyoongea danadana ziliendelea mpaka ninavyoendelea kwenye nyumba, sijawahi tena kupata jibu kutoka Vodacom. La mwisho nilijibiwa na mmoja wa watu wa Vodacom Foundation aliniabmia wewe uliingia mkataba na kampuni ya One Plass na si Vodacom Foundation.
 
SIKU YA LEO
Nimekuja  leo kuutangazia umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Account ya CRDB  ilikuwa  maalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal bank  ambayo  ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni  450,000
Nawalipa  nurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000. Maisha ya ulemavu ni ghali  sikutarajia . nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa la saba  mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili.
Hawa  wanasoma primary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila mmoja kwa  term jumla 400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka. Gharama chakula,  vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogondogo na za kifamilia Pamoja na  chakula kwa mwezi , inakwenda kati ya 750,000 mpaka 900,000 kwa mwezi.
Nimekuwa  ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala  kujibu sms  . siyo siri ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa  kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana  kiuchumi.
Sina  uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athumani Hamisi,  naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa  madaktari walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali  kulingana na hali yangu.
Makampuni  , mashirika, wizara yoyote, shirika la nyumba la Taifa NHC, watu  binafsi, serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu  nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote . kwa walio tayari  naomba misaada  ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No  010-00090488 ya Postal Bank
Kwa  wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia M-pesa 0757 825 737,  Tigopesa 0655 531 188 na Airtel Money 0784 531 118; M-Pesa 0767 298 888  ya Chris Mahundi na Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru
Athumani Hamisi