Pages

Saturday, June 9, 2012

PPRA Yazindua Zabuni Kwa njia ya Simu ya Mkononi

Kaimu Mwenyekiti body ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Jaji Thomas Mihayo (Katikati) akizindua utaratibu wa kutangaza zabuni kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya PPRA jana. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Push Media Mobile, Fredd Manento na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk Ramadhani Mlinga.
----
KATIKA vita ya kuondoa rushwa nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imezindua huduma ya njia ya simu ya mkononi kwa waombaji wa zabuni mbali mbali zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Uzinduzi huo uliofanyika juzi makao makuu ya PPRA chini ya Jaji Thomas Mihayo ambaye aliwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba zabuni hizo na siyo kulalamika zabuni hizo zinatolewa kwa upendeleo na zaidi makampuni ya nje ya nchi.

Jaji Mihayo ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa bodi ya PPRA alitolea mfano zabuni za kufua umeme hapa nchini na ile ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambazo zilileta usumbufu mkubwa na kuwa gumzo katika vyomo vya habari na jamii kwa ujumla.

“Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau wetu na vile vile kutokana na watanzania wengi kushindwa kushiriki kutokana na kukosa taarifa kwa wakati muafaka, tumeingia makubaliano na kampuni ya Push Media Mobile na sasa kila Mtanzania anayetaka kupata taarifa za zabuni zetu anatakiwa kujiunga kwa kutuma neno PPRA kwenda namba 15332 na kuanza kupokea taarifa za zabuni popote Tanzania na njie ya nchi,” alisema Jaji Mihayo.

Jaji Mihayo alisema kuwa ili kuondoa tatizo hilo na kupanua wigo wa kutangaza zabuni hizo, wameamua kuweka utaratibu wa kutangaza zabuni hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi

Alisema kuwa kwa kutumia utaalam huo, kila mtu anaweza kupata taarifa kuhusiana na zabuni zetu na kuomba ili kushinda. Alisema kuwa hata kwa hata matokeo ya tenda hizo zitatangazwa kwa njia ya uumbe huo huo.
"Kila kitu hapa kitafanyika kwa njia ya mtandao bila ya upendeeleo wowote, tunaishukuru kampuni ya Push Media Mobile kwa kutuwezesha taalam huu ambao utaondoa mianya ya rushwa katika kupoke zabauni na kuchagua washindi,” alisema.
“Hii ni fursa pekee kwa watanzania kuomba zabuni zetu, lengo ni kumfikia kila Mtanzania hata aliyekuwa vijijini kwa wakati muafaka,” alisema.

Popular Posts