Ndugu  Ridhwan J.  Kikwete akichangia jambo juu ya taarifa ya mapendekezo  ya  kamati ya  Uboreshaji wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha   mapinduzi (CCM)
 Mwenyekiti  wa  Kamati ya Maboresho na Uimarishaji wa Umoja wa Vijana wa  Chama Cha   Mapinduzi (CCM) Ndugu Hussein Bashe akiwasilisha Taarifa ya   Mapendekezo  ya kamati yake.
 Katibu  Mkuu wa  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu  Martin  Shigela,  akielezea jambo juu ya mapendekezo ya Kamati ya  maboresho. 
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Benno Malisa, akifafanua jambo katika kikao hicho.
 Naibu  Katibu Mkuu  (bara) wa  Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha   mapinduzi (CCM)  akifafanua jambo katika kikao hicho cha kujadili   maboresho ya umoja huo.
Wajumbe wakifuatilia taarifa ya kamati kwa umakini.
---
Vikao  hivyo  ambavyo vilianza rasmi tarehe  moja June 1, 2012. ambapo hoja   mbalimbali zimekuwa zikijadiliwa kwa kina,  ambapo vikao vilivyotangulia   vimejadili juu ya hoja ya Katiba Mpya na  suala la Muungano wa  Serikali  ya Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania.  Ambapo wajumbe  walichangia hoja  mbalimbali za msingi kwa kuzingatia  hali ya sasa ya  siasa nchini na  matukio sambamba na hoja hiyo, kama  vile mijadala  ndani ya majukwaa  mbalimbali juu ya muundo wa Katiba ya  sasa,  mapungufu yake na mchakato  mzima wa kupata Katiba Mpya na pia  mijadala  juu ya maboresho ya  Muungano.
Pamoja na hayo, kikao kiliadili juu ya mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha na  kuboresho Umoja huo wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mapendekezo  hayo juu ya  jinsi ya kuboresho  umoja huo yametolewa na Kamati maalum  ambayo ilipewa  jukumu la  kupendekeza namna ya kuiboresha UVCCM katika  kikao cha  Baraza hili  kilichokaliwa mnamo tarehe 19/03/2011, ili iweze  kukidhi  mahitaji ya  Siasa za ushindani wa sasa na baadae.