MTOTO OBEDI MANASE (8) MAREHEMU ALIYELIPUKIWA NA BOMU PICHA NA PARDON MBWATE WA JESHI LA POLISI KIGOMA
--- 
  Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate-Jeshi la Polisi
Mwanafunzi   mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kigadye wilaya ya   Kasulu mkoani Kigoma, Abeid Manase(8), amefariki dunia hapo hapo na   wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa   kwa mkono walilokuwa wakilichezea. 
Kamanda   wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja watoto   waliojeruhiwa na bomu hilo kuwa ni wanafunzi wawili wa darasa la kwanza   Tuju Seluke(7) aliyejeruhiwa tumboni na Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa   kwenye paja na mguu kulia. wote wanafunzi wa darasa la kwanza katika   shule ya msingi Kigadye wilayani Kasulu.
Kamanda   huyo amewata wengine waliojeruhiwa kuwa ni watoto wadogo wenye umri wa   miaka minne kila mmoja ambao walikuwa wakichezea bomu hilo kwa pamoja   ambao ni Enjord Seluke aliyejeruhiwa kwenye sikio la upande wa kushoto   na Isaka Yohana aliyejeruhiwa kwenye jicho la upande wa kushoto.
Kamanda   Kashai amesema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni   iliyopo katika kijiji cha Shunge wilauani Kasulu kwa matibabu zaidi na   hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.
Kamanda   Kashai amesema jana majira ya saa 11.00 jioni, huko katika kijiji cha   Kigadye, watoto hao walikuwa wakilichezea bomu hilo la kutupa kwa mkono   na ndipo lilipowalipukia na kumuua mwenzao na wengine hao wane   wakajeruhiwa.
Bomu  hilo lilikuwa limefichwa katika  moja ya bustani nyumbani kwa Bw. Ayoub  James Luvahovi mkazi wa kijiji  cha Kidae na likimbia mara baada ya  tukio hilo na Polisi wanamsaka. 
Katika   tukio linguine Kamanda Kashai amesema huko Kasulu, watu wenye  silahawamemjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni mfanyabiashara mmoja Bi.  Deothera  Malusha(23) na baadaye kumpora shilingi 150,000 pamoja na simu  yake ya  mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 55,000.
Amesema   baada ya uporaji huwo, majambazi hayo yalikimbia na kutokomea katika   msituni na majeruhi amelazwa kwenye Hospitali ya wilaya ya kasulu mkoni   Kigoma na hali yake bado sio nzuri.
Wakati   huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhamiaji   haramu 52 kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini bila ya kibali. 
Kamanda   Kashai amesema kuwa wayuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo  mbalimbali  walipokuwa wakifanya shughuli za uvuvi mkoani humo.