Pages

Sunday, June 3, 2012

Kikosi Cha Taifa Stars Kinavyojifua Huko Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny

Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa ‘Kilimanjaro Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa wa kituo cha Michezo mjini Abidjan juzi kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika kesho Juni 02, 2012 kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ‘Kilimanjaro Taifa Stars’ wakijifua kwenye uwanja wa kituo cha michezo mjini Abidjan juzi kujiandaa na mechi ya mchujo wa kushiriki kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny. Kulia ni Kocha Msaidizi wa timu hiyo.
Kocha wa timu ya Soka ya Taifa ya ‘Kilimanjaro Taifa Stars’, Kim Poulsen akiwapa mazoezi ya viungo wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa kiruo cha Michezo mjini Abidjan juzi kujiandaa na michuano yamchujo wa kucheza kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho Juni 2, 2012 kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
-----
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu.
Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.
Licha ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
“Tunaiheshimu Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.
Kikosi cha Stars kinaongozwa na nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris. Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.
Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.
Mbali ya Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Msafara wa Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupoMwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi hiyo.

Popular Posts