Mfanyakazi wa TBL, akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kifaa cha kuzuia vumbi kabla ya kuanza kufanya usafi.
 Mkuu  wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL  wakifagia  ikiwa ni ishara ya kuzindua rfasmi maadhimisho hayo  karibu na  Soko la  Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.
 Baadhi  ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiungana na   watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya usafi wa mazingira katika   makutano Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Muheza, Karikaoo, Dar es Salaam   jana. TBL ilitoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil. 12   kwa Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya   Mazingira, Dar es Salaam jana. 
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (katikati), akizoa taka wakati wa kampeni hiyo ya usafi wa mazingira
 Watumishi wa Manispaa ya Ilala na Wafanyakazi wa TBL, wakifanya usafi kwenye Mtaa wa Muheza, Kariakoo.
 Mkurugenzi  wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo  (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi,  msaada wa  vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya  Manispaa  ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar  es  Salaam jana.
 Mkuu  wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiendesha moja kati ya matolori   yaliyotolewa msaada na TBL kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Steve   Kilindo wa TBL.
Mtaa wa Muheza, Kariakoo ukipendeza baada ya kufanyiwa usafi.