Balozi  wa Uingereza Nchini Tanzania, Bi. Diane Corner (kushoto)  akisisitiza  jambo kwenye kikao alichofanya na Waziri wa Nishati na  Madini Mhe.  Profesa Sospeter Muhongo (katikati) mara baada ya kufanya  ziara kwenye  Wizara. Anayesikiliza upande wa  kulia ni Naibu Waziri wa  Nishati na  Madini anayeshughulikia masuala ya madini, Mhe. Stephen   Maselle. Lengo  la ziara yake ilikuwa ni kuimarisha ushirikiano baina ya  Tanzania na  Uingereza hususan katika sekta  za nishati na madini.
  Waziri wa Nishati  na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza   kwa makini Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bi. Diane Corner   katika  kikao hicho. Kikao hicho kilihusisha  pia wataalamu wa  Wizara  ya  Nishati  na Madini.