Pages

Wednesday, June 6, 2012

Language, Meaning in Editorial Cartoons

Editorial cartooning is graphic communication that mostly employs drawn images. But the form of art's most distinguishing characteristic is its ability to fuse image and text. Reading visual characteristics alone in an editorial cartoon is therefore not enough. Text is an important part of cartoons as words support images to create meaning.

Text is used in many different ways and includes captions underneath the composition. Cartoonists often use speech bubbles to attribute spoken words to one or more of the drawn figures in their compositions.

Because the human eye is trained to read from left to right, editorial cartoonists logically arrange the speech bubbles such that whatever is placed on the extreme right of the composition concludes, summarises or gives the context for the editorial cartoon.

More often than not, the bubble placed on the extreme right gives the 'punch line' to the cartoon and determines if the composition is meant to be humourous, serious, thought-provoking, or meant to be just a gag.

Other cartoonists, such as the Chronicle's Wellington Musapenda regularly replaces speech bubbles with captions as part of an artistic style that is easy to understand for the reader as they make sure the images are cleverly arranged to identify the speaker and the effect of the words to other components of the composition.

Text is also used through newspaper banners as a compass reference to the topic the editorial cartoon may be alluding to.

This makes it easier for the reader to understand the cartoon as it refers to information already in the public domain.

Cartoonists also use text as labels and signs. This technique is particularly vital where metaphorical representations are made.

Others with a vague or abstract artistic style may use labels to ensure that there is no ambiguity in both the figure drawn and the combined meaning of the editorial cartoon.

Text may be used in many ways but its meaning may be found in multiple layers.

Words can have several meanings, including conceptual, connotative, stylistic and affective implications. The conceptual meaning or sense is the logical or denotative content of the text.

It is the basic and central meaning in linguistic communication. In other words conceptual meaning is the 'dictionary' definition of a text. In this form of meaning, the word 'President' would only refer to a head of state, organisation or society who is given that title.

Connotative meaning, is cultural-based, it is the lexical meaning related to the certain thing it refers to.

In Zimbabwe, 'President' in a local cartoon automatically makes reference to the Head of State and Commander-in-Chief of the defence forces.

It would probably mean something else if mentioned in a cartoon appearing in an MDC-T newsletter for example.

Language is just as dynamic as culture and evolves within specific geographical areas such that its meaning there becomes exclusive to a local population.

Nowhere else in the world except here would the phrase 'heavy stuff' mean something appealing or pleasing to any of the human senses?

Stylistic meaning, a form of associative meaning, and referring to what a piece of language conveys about the social circumstances surrounding its use. 'Chinja' would normally mean 'change' but if used in Zimbabwe, it is a political slogan that is associated with the party led by Morgan Tsvangirai.

When 'pamberi neZanu' is translated into English, it means very little because it refers to an ideology whose social significance has no direct comparison in any other language.

There are a lot of editorial cartoonists that create their work for a global audience and succeed in doing so, but most cartoons, based on the image and textual references, only appeal to a limited audience.

Affective meaning relates to language that reflects the personal feelings of the speaker, including his/her attitude to the listener or his/her attitude towards something he/she is talking about.

Affective meaning is the emotional content of the text. When a woman is depicted in an editorial cartoon yelling to her husband, "You are a dog!" the immediate implication, as suggested by the exclamation mark is that she would be speaking in a loud high pitched voice.

Additionally, likening a man to an animal known for its low moral standards gives an indication of the woman's emotional state.

While the image representations may also show signs of a strained relationship, the text would provide an emotionally charged rant that shows her anger, her disappointment and her disproval of the man's actions.

Most cartoonists prefer to use very little text in their work mainly because their styles are effective enough to how moods, emotions, movement, action and coherence.

But whenever text is employed, it is often so little, yet so effective that the targeted audience consumes it and get understanding with minimal efforts.

This is because they carefully choose what to write so that textual meaning is immediately apparent, understood within the context and its emotional value is well considered.

Spika Mpya wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Banbtonbg Zziwa

Spika Mpya wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Margaret Banbtonbg Zziwa (49) kutoka Uganda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo uliopo katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo. Zziwa ambaye ni Mchumi kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote.

Ziara Ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye Mkoani Njombe

Msafara wa Nape ukiongozwa na pikipiki wakati ukiingia mjini Njombe kwa ajili ya mkutano wa hadhara na kufungua matawi kadhaa aya CCM
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadahara katika Uwanja wa Turbo, mjini Njombe, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo, leo 5/6/2012
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadahara katika Uwanja wa Turbo, mjini Njombe, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo, leo 5/6/2012
Nape akizindua shina la wakereketwa wa CCM la Melizine mjini Njombe wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akicharaza ngoma wakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Mlangali mkoani Njombe juzi 4/6/2012.Picha na Mdau Bashir Nkromo

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wala Kiapo

Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo
Shy Rose Banji akitia saini nyaraka za kiapo.
Mh. Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania
Mh.Charles Makongoro Nyerere
Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi
Mh. Alhaji. Adam Kimbisa
Mhe Bernard Musomi Murunyana
Dkt Twaha Issa Taslima
Mh.Nderkindo Perpetua Kessy
Mhe. Anjela Charless Kizigha.Picha Zote Zimeletwa Hapa na Mdau Mroki Mroki
---
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda

TBL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI ILALA

Mfanyakazi wa TBL, akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kifaa cha kuzuia vumbi kabla ya kuanza kufanya usafi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL wakifagia ikiwa ni ishara ya kuzindua rfasmi maadhimisho hayo karibu na Soko la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiungana na watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya usafi wa mazingira katika makutano Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Muheza, Karikaoo, Dar es Salaam jana. TBL ilitoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil. 12 kwa Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira, Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (katikati), akizoa taka wakati wa kampeni hiyo ya usafi wa mazingira
Watumishi wa Manispaa ya Ilala na Wafanyakazi wa TBL, wakifanya usafi kwenye Mtaa wa Muheza, Kariakoo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya Manispaa ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiendesha moja kati ya matolori yaliyotolewa msaada na TBL kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Steve Kilindo wa TBL.
Mtaa wa Muheza, Kariakoo ukipendeza baada ya kufanyiwa usafi.

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AAGANA NA BALOZI WA CANADA ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika Ofisini kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika Ofisini kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi CUF Yalaani Taarifa ya UVCCM

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)
JUMUIYA YA VIJANA - JUVICUF
Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk Homepage: www.cuftz.org


Our Ref: CUF/HQ/JUVICUF/003/2012/Vol 13 Date: 06/06/2012


Jumuiya ya vijana ya Chama cha Wananchi CUF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kikao cha baraza kuu la UVCCM iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu wake Martin Shigella kuhusiana na vurugu zilizotokea Zanzibar hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoitoa amesema, serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar inahusika na vurugu hizo.


Sisi vijana wa JUVICUF tunalaani kauli hiyo kwani juhudi za kuipata serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haikuwa kazi nyepesi jambo ambalo linajulikana na wazanzibari, watanzania na ulimwengu mzima. Serikali ya umoja wa kitaifa imepataikana kwa taabu nyingi baada ya Zanzibar kupoteza muelekeo wake, ustawi wake na roho za watu wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe Dr Ali Moh’d Shein alitoa taarifa rasmi kuhusiana na vurugu hizo. Kauli hiyo ya UVCCM ambayo imejaa shutuma dhidi ya serikali ya Dr Shein anayoiongoza, ambayo imekuja mara baada Rais wa kutoa taarifa yake rasmi kuhusiana na vurugu hizo ni ya utovu wa nidhamu wa wazi unaopaswa kulaaniwa na kukaripiwa kwani inaweza kuwa ni sawa na cheche ya moto katika nyasi kavu. Kuvurugika kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambayo inafanya kazi zake kikatiba na kuaminiana ni kurejesha nyuma umoja na maendeleo yaliyopatikana.

JUVICUF inatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao. Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi. Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………….
Khalifa Abdalla Ali
KATIBU MKUU

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Upande wa Tanzania Wajipongeza Baada Ya Kula Viapo

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania EALA, Alhaji. Adam Kimbisa akinon'goneza Katibu wake Shy-Rose Banji jambo wakati wa ufunguzi wa tafrija yao.
'Kaka wa Taifa' Makongoro Nyerere akitoa neno la shukrani kwa wageni wote waliohudhuria hapo. Pamoja nae ni Dkt Twaha Issa Taslima
Awali mama Maria Nyerere alihudhuria sherehe za Kuapishwa Wabunge hao ambapo Mtoto wake Charles Makongoro Nyerere nae aliapishwa kulitumikia Bunge hilo.
Shy-Rose Banji akipongezwa na ndugu na jamaa zake.
Wabunge wakipongezana baada ya kiapo nje ya Ukumbi huo wa Bunge uliopo Jengo la AICC mjini Arusha
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Shy Rose.
Picha ya marafiki na familia
'Kaka wa Taifa' Makongoro Nyerere akitoa neno la shukrani kwa wageni wote waliohudhuria hapo. Pamoja nae ni Dkt Twaha Issa Taslima
Abdula Mwinyi na Mkewe kati pamoja na Mbunge wa Bunge la Tanzania, Magige wakipata msosi
Waheshimiwa hawa nao walikuwepo...
Lady Jay Dee akifungua shampaing na kuwamiminia watu.
Wakati wa Chiiiiiiiizz!!
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki upande wa Tanzania jana usiku mara baada ya sherehe za Kuapishwa na uzinduzi wa Bunge hilo jipya la tatu walifanya sherehe ndogo ya kujipongeza iliyofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace ya mjini hapa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwapo ndugu jamaa na marafiki.Picha Zote na Mdau Mroki-Arusha

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

Ndg. Waandishi wa Habari

Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake
katika Bajeti Mbadalaambavyo vilikuwa:

1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%

2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili
kupunguza mfumuko wa bei

3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).

4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL)
kwenye bodi ya mikopoya elimu ya juu.

Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli
iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

Mapendekezo mawili,

(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na

(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya
kodi lilikubaliwa lakiniSerikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo
la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali
imeshindwa kutekeleza ahadiyake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya
kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa.Halikadhalika Kambi
ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za
vikao(sitting allowances)

Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13
trillion. Hata hivyo ni dhahirikwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina
changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezajekutekeleza
Bajeti ya 15trillioni?

Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika
maeneo yafuatayo nakuishinikiza Serikali kuyatekeleza.

1.Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya
Pato la Taifa. Hivi sasamisamaha ya kodi ni sawa na misaada yote
kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% yaPato la
Taifa.

2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga
miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.

3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia
za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.

4.Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy)
ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma.
Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3itaenda VETA na vyuo vya
Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto yamikopo
kwa wanafunzi.

5.Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili
kuwezesha wananchi wa haliya chini kubaki na fedha za kutumia na
kukuza uchumi.

6.Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa
kuhakikisha mapato ya ndaniyanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza
nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidikwenye
kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na
gesi.

7.Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.

8.Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili
kushusha mfumuko wabei.

9.Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika
kutoa elimu kwa ubora zaidi,ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa
Elimu(Regulatory authority)

10.Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani
vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira
kama Korosho,Pamba na Mkonge.

Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua
kwa deni la Taifa
amabalolimefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum
kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.

Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi
yasiyo na tija ya Serikali hasakwenye magari na posho mbalimbali na
Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa yamaendeleo ili kukuza
ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango
waMaendeleo wa Miaka mitano

Asanteni sana!…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb) Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.

Tuesday, June 5, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 5,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa China nchini, Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Juni 5,2012.Picha na Ofisi Ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akutana na Balozi wa Canada Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago cha faru, Balozi wa Canada nchini, Robert Orr ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar salaam Juni 5,2012 kuaga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Afisa wa Masuala ya Siasa katika ubalozi wa Canada nchini, Sebastien Lanthier (kulia) na balozi wake, Robert Orr (katikati) ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kuaga, Juni 5,2012.

MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AAGANA NA BALOZI WA MSUMBIJI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Amour Zacarias Kupela, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 05, 2012 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Amour Zacarias Kupela, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 05, 2012 kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
--
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumanne ya Tarehe 05 Juni 2012 amekutana na Mabalozi wa nchi za Sudan na Msumbiji waliomtembelea ofisini kake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa kwanza kufika alikuwa Balozi wa Sudan nchini Tanzania Mheshimiwa Dkt. Yassir Mohamed Ali ambaye amekutana na Makamu wa Rais kwa mara ya kwanza na katika kujitambulisha kwake akaelezea nafasi ya Tanzania katika kuhakikisha Bara la Afrika linabakia kuwa na amani na utulivu.
Balozi Mohammed alimwambia Makamu wa Rais kuwa wafanyabiashara kutoka Sudan wamekuwa wakishiriki katika uwekezaji nchini na bado wapo ambao wana nia ya kufanya hivyo na kwa kuanzia wafanyabiashara hao watashiriki katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Saba Saba yatakayofanyika mwaka huu. Balozi huyo alieleza pia kuwa, Sudan inadumisha uhusiano wake na Tanzania katika kuhakikisha nchi mbili zinabakia kuwa na lengo moja kubwa la kuwapatia wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais, yeye alimkaribisha Balozi Mohammed na kumwahidi kuwa Tanzania itazidi kutumia nafasi yake katika kuhamasisha amani hasa sasa ambapo nchi ya Sudan iko katika mgogoro na Sudan ya Kusini.
Balozi Amour Zacarias Kupela wa Msumbiji, yeye sambamba na kumuaga Mheshimiwa Makamu wa Rais alimwambia kuwa amefurahi sana kuwepo nchini Tanzania na kwamba anaithamini nchi hii kama nyumbani kutokana na uwezo wake wa kudumisha amani na pia kwa nafasi yake katika kuhakikisha wananchi wa Msumbiji wanakuwa huru na wanaishi kwa amani kama ilivyo sasa.
Balozi huyo alisema serikali ya Msumbiji inatumia fursa zake za kuhakikisha inakuza kilimo ili kutoa nafasi ya kuwepo chakula cha kutosha nchini humo na
pia akafafanua kuwa hali ya kisiasa nchini mwake kwa sasa ni shwari na hivyo wananchi wa ajukumu moja tu la kujitafutia maendeleo.
Balozi Maricias alifafanua kuwa upo umuhimu wa kukuza nafasi za kubadilishana wanafunzi kati ya Msumbiji na Tanzania kwani kama haitafanyika hivyo ni rahisi wananchi wa nchi hizi kusahau historia ya namna nchi hizi mbili zilivyoshirikiana katika kipindi cha kupigania uhuru.
Makamu wa Rais alimueleza Balozi Maricias kuwa, Tanzania inashukuru sana kwa mchango wake alioutoa kama Balozi na pia katika kazi alizofanya kabla ya kuwa Balozi. Alimtakia kila la kheri katika kazi zake mpya huku akimhakikishia kuwa Tanzania itabakia na mahusiano chanya na Msumbiji katika kipindi chote.
Imetolewa:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM

Popular Posts